Neno kutoka kwa CEO

Afande CNS

“Lengo kuu la SUMAJKT ni kufanikisha mpango wa maendeleo  sambamba na dhumuni la serikali katika kuufikisha uchumi wa viwanda katika kuviimarisha viwanda vilivyopo na vingine vipya

SUMAJKT inapanua ushurikiano wake na taasisi za kifedha kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi mipya ikijumuisha miradi ya kimkakati katika ujenzi, uhandisi na usanifu, kilimo, mifugo, sekta ya uvuvi, sekta ya viwanda, biashara, sekta ya huduma pamoja na elimu.

Katika mpanngo mkakati wake wa miaka mitano, SUMAJKT litahakikisha kwamba uwekezaji katika nyanja zilizotajwa hapo juu zitakamilishwa kikamilifu bila kujali misukumo kutoka nje. Uongozi utafanya kazi na wadau muhimu wa maendeleo . Fedha imekuwa ni chagizo muhimu katika kufikia mipango ya shirika , hata hivyo, mpango uliowekwa ni kuongeza fursa za kibiashara ili  kulipa shirika misuli ya kiuchumi ili kuendeleza miradi ya SUMAJKT ili kuendana na kasi ya mpango wa miaka mitano wa Taifa.

Vilevile uongozi utaendeleza juhudi za kutafuta mali-fedha kama nyenzo muhimu ya kutekeleza shughuli za kimkakati ili kufikia lengo.

Mwisho, SUMAJKT inapenda kuwashukuru wabia ambao kwa namna moja au nyingine wanahakikisha shughuli za shirika zinakwenda kama zilivyopangwa.”

Kuhusu SUMAJKT

Shirika hili lilianzishwa tarehe 01 Julai 1981 kwa Sheria ya Uanzishwaji Mashirika ya Kibiashara katika Taasisi za Umma (The Corporation Sole (Establishment) Act, (Cap 119 RE 2002).
Shirika lilianzishwa kwa lengo la kufanya biashara na kuzalisha faida ili kuchangia gharama za kuendesha shughuli za JKT pamoja na kujenga uchumi wa Taifa.

DIRA YETU

Kuwa shirika kubwa, lenye sifa kibiashara na litakalokuwa na uwezo wa kusaidia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuendesha shughuli zake.

DHIMA YETU

Kuanzisha na kuendesha shughuli za uzalishaji mali na huduma kwa tija katika sekta za kilimo, ulinzi, uhandisi na ujenzi, viwanda na biashara pia kutoa huduma kwa ufanisi, ubora na weledi.

 

SHUGHULI MBALIMBALI ZA UZALISHAJI MALI NDANI YA SUMAJKT

Miradi mingine ya shirika

    

Mradi upo eneo la Mwenge Jijini Dar es Salaam. Mradi huu ni matokeo ya juhudi za Serikali zilizofanywa katika kutekeleza mpango wa kuinua sekta ya kilimo kupitia kauli mbiu ya “Kilimo Kwanza” mwaka 2009 kutokana na juhudi za Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.

Shirika katika mpango huo lilipewa jukumu la kupokea kutoka Serikalini na kusambaza matrekta na zana za kilimo zilizonunuliwa kutoka nje. Hivyo, JKT kupitia Shirika lilianzisha mradi wa matrekta ili kutekeleza jukumu hilo la Serikali.

zana za umwagiliaji

Mradi huu umekuwa msaada kwa wakulima tangu kuanzishwa kwake kwani wengi wamefaidika kupitia huduma ya Matrekta na zana zake. Aidha, huduma ya kusambaza matrekta, zana na vipuri vyake umesaidia kuanzisha mradi wezeshi wa kuuza matrekta, vipuri na zana za kilimo kwa njia ya fedha taslimu. Matrekta na zana hizo ni; Matrekta ya New Holland na FARMTRAC, majembe ya kulimia (Disc Plough), jembe la kuvunja udongo (Disc harrow), pump za umwagiliaji (Irrigation water pump) na tela (Trailer).

Mradi huu umewawezesha wakulima nchini kufaidika kwa kupata uelewa wa matumizi juu ya zana za kilimo, kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na ajira hasa maeneo ya vijijini.

Tembele tovuti yetu ya SUMAJKT Agrimachirery kufahamu zaidi.

Jengo la kitega uchumi SUMAJKT HOUSE la Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo Medeli mashariki jijini Dodoma. Jengo limejengwa kwa dhumuni la kupangisha wateja mbalimbali kama ofisi na shughuli nyingine za kiuchumi.[/caption]

Mradi huu unahusika na kununua, kunenepesha, kuchinja na kuuza nyama yenye ubora kwa bei nafuu katika baadhi ya vikosi vya JKT pamoja na maeneo mbalimbali yaliyopo katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Mradi huu ulianza kufanya kazi tarehe 01 Mei 2017 katika vikosi vya 832KJ Ruvu, 833KJ Mgambo pamoja na 841KJ Mafinga.

Mradi unaendelea kufanya vizuri ili kufikia malengo iliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko mengine mbali na kutegemea vikosi vya Jeshi. Matarajio ya baadae ni kuanzisha kiwanda cha nyama kwa lengo la kuiongezea thamani na kuuzwa ndani na nje ya nchi. Mradi unapanga kuchakata ngozi zitakazozalishwa na kuziongeza thamani na kuuza sehemu mbalimbali kwenye uhitaji.

makampuni tanzu

Sisi SUMAJKT tunafanya kazi katika maeneo mbalimbali kama namba zinavyoonyesha.

Makampuni Tanzu
0
Makundi ya Miradi
0
Shughuli Nyingine
0

Washitiri Wetu

Baadhi ya washitiri tunaofanya nao kazi:

FAIDI FURSA ZA KIBIASHARA KUTOKA SUMAJKT

Shirika letu linakaribisha wadau kutoka sekta mbalimbali za kiuchumi kushirikiana nasi katika biashara ili kufungua milango ya fursa kwa Watanzania wote.