Neno la CEO

“Tunajizatiti kuhakikisha SUMAJKT linakuwa shirika bora na lenye ushindani ndani na nje ya Tanzania. Kimsingi, tunachotaka kufanya SUMAJKT ni rahisi kueleza , tunataka kuona mchango wetu katika maendeleo ya taifa unaonekana kwa vitendo.

Tunaendana na dira ya nchi ya kujenga uchumi wa viwanda, lakini hatuishii hapo. Tunaangalia pia mazingira yanavyobadilika, tunajiuliza maswali, na pale tunapoona nafasi ya kutekeleza zaidi, tunachukua hatua. Si tu kulinda tulichonacho, bali kukikuza na wakati mwingine kujaribu kabisa mwelekeo mpya.

Hata hivyo, hatukusubiri hali iwe tulivu ndipo tuanze kupanga. Tumeamua kusonga mbele huku tukishirikiana kwa karibu na wadau wetu, kwa sababu tunaamini bila ushirikiano, mambo mengi hayafiki mbali.


Kwa upande mwingine, tuna matumaini lakini sio ya kujifurahisha tu. Tunaamini fursa za kibiashara zitaendelea kujitokeza na kutupa nafasi ya kujiimarisha kifedha. Pamoja na hilo, hatutegemei njia moja pekee. Tutaendelea kutafuta njia nyingine, hata zile ambazo hatujazoea sana, ili kuhakikisha kazi zinaendelea hata pale rasilimali zinapokuwa finyu.


Ni vizuri pia kusema kuwa Mawazo haya si kazi ya mtu mmoja. Umetokana na mawazo ya wengi, majadiliano ya hapa na pale, na juhudi za pamoja. Kuna dhamira ya kweli ya kuona SUMAJKT inasonga mbele na si kwa ukubwa tu, bali pia kwa ubora na heshima yake. Lakini mwisho wa siku, mafanikio hayatatokana na maandishi haya, bali yatatokana na namna tutakavyoyasimamia na kuyatekeleza.


Mwisho kabisa, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wadau na wateja wetu we huduma na biashara tunazoazitoa. Na kwa namna ya pekee, nawapongeza uongozi na watendaji wa SUMAJKT kwa kujitoa kwao bila juhudi hizo, kazi hii isingefika hapa ilipo.”

.

Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele

Afisa Mtendaji Mkuu, SUMAJKT.

Habari Mpya

1981
Kuanzishwa
100110+
Idadi ya Wateja
21
Kampuni Tanzu
Kujisajili gusa picha hii.

Sekta 5 za Kimkakati ndani ya SUMAJKT

Malengo Yetu

Dira (Vision)

Kuwa taasisi ya kibiashara ya sekta mbalimbali iliyo kinara na yenye sifa njema, inayochochea ukuaji endelevu na ubunifu, huku ikiunga mkono Jeshi la Kujenga Taifa na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

Dhima (Mission)

Kubuni, kuendeleza na kusimamia miradi yenye ufanisi, ubunifu na tija ya kibiashara katika sekta mbalimbali, kwa kuzingatia utaalamu na matumizi bora ya rasilimali, kwa manufaa ya Jeshi la Kujenga Taifa na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Kuwasiliana nasi, tafadhali gusa kitufe hapa chini.