Kwa sasa Shirika linaendesha shughuli za ufugaji katika baadhi ya makambi na vikosi vya JKT. Kwa kuzingatia mkakati wa JKT kujitosheleza kwa chakula na Shirika kujiendesha kibiashara, mgawanyo wa rasilimali mifugo ulifanyika mwaka 2017 katika shamba la Mifugo Oljoro (833 KJ) Mkoani Arusha. Shamba hili linafuga ng’ombe wa nyama na maziwa na shamba la mifugo Mafinga (841 KJ) Mkoani Iringa, ambalo huzalisha maziwa pamoja na kufanya biashara ya kuuza mitamba. Aidha, Shirika linafuga katika Huria ya Misenyi ndani ya Kiteule cha Misenyi mkoani Kagera ambapo linafuga ng’ombe wa nyama aina ya Ankole, mbuzi na kondoo. Shirika linaboresha na kufuga kitaalamu ili kukidhi mahitaji ya soko.