SUMAJKT Port Services

Hii ni kampuni ya Shirika iliyosajiliwa rasmi mwaka 2020 kwa lengo la kusimamia shughuli za upakiaji na upakuaji wa mizigo bandarini na kuhakikisha usalama wa bidhaa zinazoingia na kutoka nchini.

Mwaka 2017, ilianza kutoa huduma ya kuratibu na kusimamia wafanyakazi wa kutwa wanaoingia kufanya kazi ndani ya bandari ya Dar es Salaam.

Mwaka 2019, mradi ulipewa kazi ya kutoa huduma hiyo katika bandari za Kigoma na Mwanza. Kwa sasa, imeingia makubaliano mapya ya kuratibu na kusimamia wafanyakazi katika bandari zote zilizopo chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambazo ni bandari za Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Mtwara, Kigoma, Kyela, Kasanga, Bukoba na Kemondo.

Kampuni inaendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu katika kutoa huduma na kujenga imani kwa watumiaji wa bandari zote nchini baada ya kuamini kuwa ni sehemu salama ya kupitishia mizigo yao.

Fanya kazi nasi leo

Kwa huduma bora ya forodha pamoja na shughulli za Bandarini, usisite kuwasiliana nasi kupitia njia hizi:

P.O . BOX 1694,
Dar Es Salaam, Tanzania.

Simu/WhatsApp: +255 738 133 505

email: sumajktportservices@sumajkt.go.tz

au fika ofisini kwetu jijini Dar es salaam.