Shughuli za uzalishaji kupitia kilimo zinaendeshwa kwenye maeneo mbalimbali ya Makambi na vikosi vya JKT. Kwa sasa, shughuli hizi husimamiwa na mameneja kwenye maeneo husika tofauti na hapo awali ambapo makamanda vikosi walikuwa wakisimamia shughuli hizo. Shirika linaendelea kupanua shughuli za kilimo kwa kutafuta mashamba mapya na yale yanayotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) kwa lengo la kuyaendeleza kibiashara.
Shirika linazalisha shamba la mbegu za maua ya aina mbalimbali katika shamba la USA River mkoani Arusha.