SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI LA KUJENGA TAIFA
(SUMAJKT)

Kawawa Secondary School

Shule ya Sekondari Kawawa ilianzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kutoa elimu kwa maafisa, askari, familia za askari na raia wa maeneo jirani na shule. Ujenzi ulianza mwezi Agosti 1992, ukifanywa na maafisa, askari wa Kikosi cha Jeshi 841 Mafinga JKT. Shule hii ipo ndani ya Kikosi cha jeshi 841 Mafinga.

Shule ni ya mchanganyiko (wasichana na wavulana) na hutoa huduma ya bweni na kutwa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita. Shule ilisajiliwa kwa mchepuo wa kilimo kwa kidato cha kwanza hadi cha nne. Aidha, mwaka 2008 shule ilipata kibali cha kuanzisha kidato cha tano na sita kwa tahasusi ya sanaa (HGK, HGL na HKL). Pia, mwaka 2022 shule ilianzisha shule ya awali na shule ya msingi (Kawawa JKT Pre & Primary School).

Mnamo tarehe 10 Novemba 2018 shule ilikabidhiwa SUMAJKT ili kuiendesha kibiashara.

Wizara ya Ulinzi

Jeshi la Wananchi la Tanzania

Jeshi la Kujenga Taifa

Shirika La Nyumbu

SUMAJKT© 2023

Imewezeshwa na Kutengenezwa na SUMAJKT

linkedin facebook pinterest youtube rss twitter instagram facebook-blank rss-blank linkedin-blank pinterest youtube twitter instagram