Jitegemee Sekondari ni shule ya wavulana na wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Shule hii ni ya Kutwa Pamoja na huduma ya malazi kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule, pamoja na wale wenye mahitaji maalumu yanayotokana na mazingira yao ya kifamilia yasiyotoa nafasi nzuri ya mwanafunzi kujisomea.
Chimbuko la shule hii ni Sera ya Elimu ya Watu Wazima ambapo mwaka 1974 ilisajiliwa kama Kituo cha Elimu ya Watu Wazima kikitoa elimu ya sekondari kwa maafisa na askari. Kwa wakati huo, Shule iliitwa Mgulani (JKT) Sekondari. Baada ya kuwa na ongezeko kubwa la Maafisa na Askari waliopata elimu ya sekondari na mahitaji ya wazazi, Sera ya elimu ndani ya Jeshi ilibadilishwa. Kutokana na mabadiliko hayo mwaka 1985 shule ilisajiliwa kutoa elimu ya sekondari kwa wanafunzi wote. Mnamo mwaka 2019 shule ilikabidhiwa SUMAJKT ili kuiendesha kibiashara.