SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI LA KUJENGA TAIFA
(SUMAJKT)

Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

Kilimo

Shughuli za uzalishaji kupitia kilimo zinaendeshwa kwenye maeneo mbalimbali ya Makambi na vikosi vya JKT. Kwa sasa, shughuli hizi husimamiwa na mameneja kwenye maeneo husika tofauti na hapo awali ambapo makamanda vikosi walikuwa wakisimamia shughuli hizo. Shirika linaendelea kupanua shughuli za kilimo kwa kutafuta mashamba mapya na yale yanayotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) kwa lengo la kuyaendeleza kibiashara. 

Mwaka 2021, Shirika lilikabidhiwa shamba la ukubwa wa zaidi ya ekari 12,000 lililokuwa likijulikana kama Kilombero Plantation Limited (KPL). Kwa sasa shamba hilo linaitwa SUMAJKT Mngeta Plantation mkoani Morogoro ambako uzalishaji wa mpunga na mahindi kwa kiwango kikubwa unafanyika. Hii ni kutokana na shamba hili kuwa na miundombinu ya kisasa ya kilimo cha umwagiliaji, mashine za kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa na zinazosaidia kuhifadhi mazao ya mpunga na mahindi.

Pia, Shirika linazalisha mazao mbalimbali kama vile alizeti na maharage katika shamba lake lililopo Hanang mkoani Manyara, mpunga katika shamba la Chita (837 KJ) mkoani Morogoro, kilimo cha mahindi Milundikwa (847 KJ) mkoani Rukwa na Tanganyika Farm mkoani Katavi na mbegu za maua ya aina mbalimbali katika shamba la USA River mkoani Arusha.

Ufugaji

Kwa sasa Shirika linaendesha shughuli za ufugaji katika baadhi ya makambi na vikosi vya JKT. Kwa kuzingatia mkakati wa JKT kujitosheleza kwa chakula na Shirika kujiendesha kibiashara, mgawanyo wa rasilimali mifugo ulifanyika mwaka 2017 katika shamba la Mifugo Oljoro (833 KJ) Mkoani Arusha. Shamba hili linafuga ng’ombe wa nyama na maziwa na shamba la mifugo Mafinga (841 KJ) Mkoani Iringa, ambalo huzalisha maziwa pamoja na kufanya biashara ya kuuza mitamba. Aidha, Shirika linafuga katika Huria ya Misenyi ndani ya Kiteule cha Misenyi mkoani Kagera ambapo linafuga ng’ombe wa nyama aina ya Ankole, mbuzi na kondoo. Shirika linaboresha na kufuga kitaalamu ili kukidhi mahitaji ya soko.

Uvuvi na Ufugaji Samaki

Hapo mwanzo, Shughuli za Uvuvi zilikuwa zikifanyika katika Ziwa Victoria chini ya Kikosi cha Jeshi Rwamkoma (822KJ), kwa upande wa Ziwa Tanganyika chini ya Kikosi cha Jeshi Bulombora (821 KJ) na Bahari ya Hindi chini ya Kkikosi cha Jeshi Mbweni (836KJ). Baadaye, Shirika lilianzisha mradi wa ufugaji wa samaki unaoitwa SUMAPONICS (kwa njia ya kuzungusha maji (Recirculating Aquaculture System) katika Kikosi cha Mbweni JKT mwaka 2017. Mradi huu unazalisha vifaranga vya samaki na kuviuza kwa wahitaji pamoja na kutoa elimu ya ufugaji wa samaki kwa jamii na kuwajengea mifumo ya matenki.

Wizara ya Ulinzi

Jeshi la Wananchi la Tanzania

Jeshi la Kujenga Taifa

Shirika La Nyumbu

SUMAJKT© 2023

Imewezeshwa na Kutengenezwa na SUMAJKT

linkedin facebook pinterest youtube rss twitter instagram facebook-blank rss-blank linkedin-blank pinterest youtube twitter instagram