SUMAJKT Bottling Co. Ltd.

Kiwanda hiki kinazalisha maji ya kunywa yanayoitwa “Uhuru Peak Pure Drinking Water”, kilianzishwa rasmi tarehe 17 Aprili 2018 kwa jina la SUMAJKT Bottling Plant. Kilisajiliwa kuwa Kampuni kwa jina la SUMAJKT Bottling Co. Ltd mwaka 2020. Kiwanda kipo katika eneo la Mgulani JKT jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya kiwanda ni “The Peak of Natural Purity”.

Wazo la uanzishwaji kiwanda cha maji lilikuja baada ya SUMAJKT kutaka kufufua kiwanda kilichokuwa cha dawa za binadamu cha TANZANSINO kwa kushirikiana na Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (TSSA). Tathimini ya kitaalamu ilifanywa kwa ushirikiano wa watendaji kutoka SUMAJKT, NHIF na MSD katika eneo la TANZANSINO na kushauri kuwa eneo halikidhi vigezo vya uanzishaji wa kiwanda cha kisasa cha dawa za binadamu. Kwa kuzingatia ushauri huo Shirika liliamua kuanzisha kiwanda cha maji ya kunywa katika eneo hilo

Maji yanayozalishwa na kiwanda hiki ni sehemu muhimu ya huduma ya maji ya kunywa safi na salama inayotolewa kwa jamii vikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na watu binafsi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Bottling Co Ltd, Luteni Kanali Mtuma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu yake ya utendaji.

Uzoefu wetu

Muda kwenye biashara:

Miaka
0

Wafanyakazi waliopo

Wafanyakazi
0 +

katoni za chupa zilizozalishwa

katoni
0 +

DIRA

Kuzalisha bidhaa za viwango vya juu na zenye bei nafuu kwa mteja.

DHIMA

Kuhakikisha tunakuwa kampuni bora katika sekta ya vinywaji inayothamini viwango katika huduma za maji safi na salama.

Fanya kazi nasi leo

Tembelea ofisi zetu au chukua mawasiliano yetu haya hapa:

SUMAJKT, Bottling Co Ltd

P.O. Box 1992, Chan’gombe Area,

Plot No 321, Temeke, Dar Es Salaam, Tanzania

Tel: (+255) 769 740 744

Email: bottlingplant@sumajkt.go.tz