SUMAJKT Auction Mart Co. Ltd

SUMAJKT Auction Mart Company Limited ni Kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT yenye utaalamu na inajishughulisha na kazi za kukusanya ushuru (Levy Collection), ukusanyaji madeni (Debt Collection) na udalali wa minada (Auctioneers) baada ya kusajiliwa tarehe 11 Juni 2019.

Wazo la kuanzishwa SUMAJKT Auction Mart Co. Ltd lilitokana na Shirika kuwa na wateja ambao hawalipi madeni kwa wakati baada ya kupata huduma kutoka kampuni tanzu na hivyo kulazimika kuanzisha kampuni hii badala ya kuendelea kutumia kampuni binafsi kukusanya madeni.

SUMAJKT Consultancy

Wateja wakubwa wa kampuni hii ni Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi mbalimbali za kifedha, mashirika madogo madogo ya kifedha na kampuni za biashara. 

Mpaka sasa, kampuni imefanya kazi nyingi hasa kwenye ofisi za halmashauri za wilaya hapa nchini na mpango wa baadaye ni kuboresha huduma zake na kufikia maeneo mengine ya nchi.

DIRA

Ni kutoa huduma ya kukusanya Ushuru,Madeni na kufanya Minada yenye thamaniendelevu iliyoongozwa na ubora ikiwa na suluhisho kwa wateja, iwe ni mtu binafsi au Shirika ikiwa lengo kuu ni kukidhi hitaji la Mteja.

Maono

Kutambuliwa kama taasisi bora inayoongoza katika kukusanya Madeni,Ushuru na minada nchini Tanzania.

Majukumu

 • Kuwajibika katika kukusanya malipo ya tozo zilizopitishwa.
 • Kupanga orodha za wadaiwa kulingana na miitikio ya uurejeshaji wa madeni husika.
 • Kuwaunganisha wadaiwa na wadaiwa wao na kusimamia akaunti za wateja katika kurejesha madeni husika.
 • Kutafuta na kuwatambua wadaiwa kupitia Habari taafifa za ofisi za mikopo,hundi za nyuma,
 • Hati za mikopo na nyaraka zihusianazo na hizo kamahifadhi data.
 • Kuweka na kusimamia kumbukumbu za makubaliano mapya kama mpango mkakati kazi wa kulipa deni
 • Kushauri kitaalamu namna bora ya kukusanya deni kwa mujibu wa tafiti kulimgana na aina ya ndeni

WATEJA WETU

 

 • Serikali kuu.
 • Serikali za mitaa
 • Taasisi mbalimbali za kifedha
 • Mashirika madogo madogo ya kifedha
 • Kampuni za biashara

Fanya kazi nasi leo

Tembelea ofisi zetu au bofya kitufe hiki kupata   mawasiliano yetu..