-
Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi. Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata. Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha
-
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi ka Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amefanya mazungumzo na Jumuiya ya wafanyabiashara kisiwani Comoro katika ukumbi wa Chambre de Commerce Ngazidja uliopo kisiwani humo. Kikao hicho kimefanyika tarehe 5 Septemba 2024, na wafanyabiashara wanaochukua bidhaa Tanzania na kuzipeleka nchini Comoro, Brigedia Jenerali Ngata alipata fursa ya kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT hususani katika Sekta ya Ujenzi, Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata ameeleza nia thabiti ya SUMAJKT kuhitaji kufanya kazi na wafanyabiashara hao katika nyanja ya Ujenzi na Kilimo. Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro
-
-
Kampuni ya Umeme ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Electrical Co Ltd. Imepongezwa kwa kutekeleza kwa wakati na weledi Mkubwa kandarasi ambazo imekua ikiingia mikataba. Akizungumza Naibu waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko katika hafla ya kutia saini mkataba wa kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia katika makambi 22 ya JKT kwa mikoa 14 uliyosainiwa baina ya JKT na Wakala wa Nishati vijijini REA,Tukio lililofanyika Jijini Dodoma. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko amelipongeza Shirika la Uzalishaji Mali la JKT(SUMA JKT) kupitia SUMAJKT Electric Co.Ltd kwa
-
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujitolea kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wenye sifa za kujiunga na Jeshi hilo huku watakaopata nafasi hizo wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Novemba 1 hadi 3 Mwaka huu. Akizungumza Septemba 25, 2024 na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT,Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Kanali Juma Mrai amesema usaili utaanza Oktoba 1, mwaka huu kupitia Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar. “Mkuu wa Jeshi






