|

BRIGEDIA JENERALI NGATA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYABIASHARA NCHINI COMORO

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi ka Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amefanya mazungumzo na Jumuiya ya wafanyabiashara kisiwani Comoro katika ukumbi wa Chambre de Commerce Ngazidja uliopo kisiwani humo.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 5 Septemba 2024, na wafanyabiashara wanaochukua bidhaa Tanzania na kuzipeleka nchini Comoro, Brigedia Jenerali Ngata alipata fursa ya kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT hususani katika Sekta ya Ujenzi, Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Aidha, Brigedia Jenerali Ngata ameeleza nia thabiti ya SUMAJKT kuhitaji kufanya kazi na wafanyabiashara hao katika nyanja ya Ujenzi na Kilimo.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata akikabidhi maji ya Uhuru Peak, ikiwa ni moja ya bidhaa zinazozalishwa na shirika hilo.

Kwa upande wa wafanyabiashara kisiwani Comoro wamesema kuwa wanapenda kufanya biashara na SUMAJKT ila changamoto inayowakabili wanaponunua mifugo kutoka Tanzania inafika kisiwani Comoro ikiwa imekufa na pia wanatozwa gharama kubwa kwenye mifugo.

Akijibu kuhusu changamoto hizo, Brigedia Jenerali Ngata amefafanua kuwa SUMAJKT itaona namna ya kufanyia kazi changamoto hizo zitakazokuwa ndani ya uwezo wa shirika ili kufanya biashara itakayonufaisha pande zote mbili.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Balozi wa Tanzania kisiwani Comoro, Mheshimiwa Said Yakub.

Baada ya kikao hicho ilifanyika hafla fupi iliyoandaliwa na Gavana wa Ngazidja Mhe. Mze Ibrahimu Hamad.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT akifanya mazungumzo na wafanyabiashara alipokuwa ziarani visiwani Comoro.

SUMAJKT imekuwa ikipanua wigo wa biashara kwa kufanya mashirikiano na wadau mbalimbali kwa lengo la kuzalisha faida zaidi ili kutekeleza majukumu ya uzalishaji wake.

Kikao hicho kimefanyika kufuatia ziara ya Ujymbe kutoka SUMAJKT nchini Comoro ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Brigedia Jenerali Petro Ngata ambayo imelenga kuangalia fursa za biashara.

Similar Posts

  • JKT YATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO KWA VIJANA

    Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujiunga na Mafunzo ya kujitolea kwa vijana wa Tanzania kwa mwaka 2026/27 huku ikisisitiza kuwa nafasi hizo si za ajira, bali ni kwa ajili ya mafunzo yatakayowajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kushiriki katika shughuli za Maendeleo ya Taifa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 12, 2026 na Mkuu wa Tawi la Utawala Brigedia Jenerali Hassan Mabena kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, ni kwamba utaratibu wa kuomba na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo utasimamiwa na Ofisi za wakuu wa Mikoa na Wilaya katika maeneo wanayoishi waombaji….

  • WATANZANIA WANUFAIKA NA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SUMAJKT

    Tarehe 16 Januari 2023, Mkuu wa tawi la utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena alizindua magari 17 kwa ajili ya kuimarisha a utendaji wenye tija na kuboresha huduma za ulinzi. Aidha aliendelea kusema kwamba SUMAJKT itaendelea kutengeneza fursa mbalimbali kupitia kampuni ya SUMAJKT na hivyo kunufaisha Watanzania kwa ujumla. Bregedia Jenerali Hassan Mabena liendelea kuwashukuru na kuwaasa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuendelea kufanyakazi kwa kupitia kampuni tanzu za SUMAJKT.

  • Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electrical Co Ltd kuongezewa kandarasi za kusambaza umeme.

    Kampuni ya Umeme ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Electrical Co Ltd. Imepongezwa kwa kutekeleza kwa wakati na weledi Mkubwa kandarasi ambazo imekua ikiingia mikataba. Akizungumza Naibu waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko katika hafla ya kutia saini mkataba wa kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia katika makambi 22 ya JKT kwa mikoa 14 uliyosainiwa baina ya JKT na Wakala wa Nishati vijijini REA,Tukio lililofanyika Jijini Dodoma. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko amelipongeza Shirika la Uzalishaji Mali la JKT(SUMA JKT) kupitia SUMAJKT Electric Co.Ltd kwa…

  • Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ

    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ, kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo sasa wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpira wa magongo na mpira wa kikapu. “Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi…

  • DED SUMAJKT atembelea Mafinga.

    DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa. Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi. Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea…

  • SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

    SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *