JKT YATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO KWA VIJANA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujiunga na Mafunzo ya kujitolea kwa vijana wa Tanzania kwa mwaka 2026/27 huku ikisisitiza kuwa nafasi hizo si za ajira, bali ni kwa ajili ya mafunzo yatakayowajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kushiriki katika shughuli za Maendeleo ya Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 12, 2026 na Mkuu wa Tawi la Utawala Brigedia Jenerali Hassan Mabena kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, ni kwamba utaratibu wa kuomba na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo utasimamiwa na Ofisi za wakuu wa Mikoa na Wilaya katika maeneo wanayoishi waombaji.

JKT limeeleza kuwa vijana wenye taaluma mbalimbali hususan Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Sayansi ya Kompyuta, Usalama wa Mitandao, pamoja na Walimu wa Elimu ya Ufundi Stadi (VET) katika fani za Uchomeleaji, Ufundi Magari, Umeme, Useremala, Ushonaji, na fani nyingine, wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia mikoa yao.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *