Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amkabidhi tuzo ya Mshidi wa Jumla Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT katika sherehe za kufunga Mashindano ya #cdfcup2024 yaliyofanyika katika Uwanja wa uhuru, jijini Dar es salaam.
Similar Posts
WATANZANIA WANUFAIKA NA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SUMAJKT
Tarehe 16 Januari 2023, Mkuu wa tawi la utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena alizindua magari 17 kwa ajili ya kuimarisha a utendaji wenye tija na kuboresha huduma za ulinzi. Aidha aliendelea kusema kwamba SUMAJKT itaendelea kutengeneza fursa mbalimbali kupitia kampuni ya SUMAJKT na hivyo kunufaisha Watanzania kwa ujumla. Bregedia Jenerali Hassan Mabena liendelea kuwashukuru na kuwaasa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuendelea kufanyakazi kwa kupitia kampuni tanzu za SUMAJKT.
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi
Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Daniel Sillo ayashauri mashirika ya Kijeshi ndani ya Nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Sayansi na Teknolojia katika uzalizalishaji wa bidhaa zao. Mhe. Sillo amesema hayo leo tarehe 25 Februari 2025 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mashirika yanayo milikiwa na Majeshi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Geraffe iliyopo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi, Amefafanua kuwa Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Viwanda vilivyopo ndani ya Majeshi yaliyopo katika Jumuiya ya…
WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI KATAVI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Katavi. Katika ziara hio Waziri Mkuu alifanya ziara katika Hospitali ya rufaa mkoani Katavi. Fuatilia video hii hapa kupata taarifa zaidi.
Timu ya Mpira wa Miguu SUMAJKT yawasili Tanga kushiriki SHIMMUTA
Timu ya Mpira wa Miguu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT, imewasili Jijini Tanga hi tarehe 10 Novemba 2024, kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMMUTA) iliyoanza Kutimua vumbi katika jiji hilo. Akizungumza mara baada ya kuwasili Jijini Tanga Katibu wa Kamati ya SHIMMUTA Kapteni Kichawele Bokassa, amesema timu imejiandaa vizuri kushiriki Michuano hiyo.
SUMAJKT LAJIWEKEA MALENGO MWAKA WA FEDHA 2024/’25
Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) limeweka malengo ya kufikika na linaendelea kusimamia miradi kwa ufanisi ili kuleta tija kwa shirika. Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya (SUMAJKT) Meja Jenerali (mstaafu) Farah Mohamed, amesema hayo tarehe 19 Oktoba 2024 katika kikao cha kwanza cha malengo ya shirika cha mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa SUMAJKT Tower uliopo jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa wajumbe wa Bodi akiwemo Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata pamoja na wajumbe waalikwa…
Brigedia Jenerali Petro Ngata Ameitaka Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electric Co Ltd kuvitunza vitendea kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Brigedia Jenerali Petro Ngata Ameitaka Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electric Co Ltd kuvitunza vitendea kazi vinavyonunuliwa ili viweze kudumu na kuleta tija kwa Shirika. Amezungumza hayo Tarehe 14 Februari 2025, baada ya kufanya Uzinduzi wa Gari Jipya la utawala lililonunuliwa na Kampuni hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi. Awali akitoa taarifa fupi ya ununuzi wa gari hilo Mkurugenzi Mwendeshaji wa SUMAJKT Electric Co Ltd. Meja James Mhame, amesema kuongezeka kwa gari hilo kutarahisisha utekelezaji wa majukumu yao. SUMAJKT Electric Co.Ltd Inajishughulisha na Kandarasi mbalimbali za Miundombinu…


