Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda
Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda. Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, amefunga Kikao cha Wakuu wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo tarehe 26 Feb 2025 katika hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Salum Othman, amesema Mkutano huo huibua fursa, Masoko na namna nzuri ya kuboresha teknolojia ya Viwanda na Mashirika ya jumuiya hiyo. Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda. Akizungumza kuhusu lengo la Mkutano huo, ameeleza ni kuweka pamoja na kuimarisha ushirikiano wa Mashirika…


