𝐉𝐈𝐄𝐏𝐔𝐒𝐇𝐄𝐍𝐈 𝐍𝐀 𝐕𝐈𝐓𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐕𝐈𝐎𝐕𝐔 𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐅𝐀𝐍𝐘𝐄 𝐕𝐈𝐙𝐔𝐑𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐄𝐍𝐔.

Mkurugenzi wa Masoko SUMAJKT Luteni kanali Lucy Batakanwa amewataka wanafunzi wa jitegemee JKT Sekondari kujiepusha na vitendo viovu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo na kutimiza ndoto zao.

Luteni kanali Batakanwa ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2026 wakati wa kuhitimisha Mafunzo ya ukamavu na Uzalendo kwa wanafunzi wa kidato cha Tano na wale waliohamia katika Shule ya jitegemee Sekondari iliyopo mgulani JKT.

Kwa upande wake kaimu Makamu Mkuu wa shule hiyo Meja Geofrey Nzengele amesema mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi kwa wanafunzi wapya wanaojiunga na shule ya Sekondari Jitegemee ili kuwawezesha kujua mazingira halisi ya shule, kuwa na utayari wa kupokea amri na maelekezo mbalimbali ndani na nje ya shule.

Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya ukakamavu na Uzalendo kila mwaka kwa wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza na cha Tano kabla ya kuanza masomo yao.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *