Uncategorized

  • CDF MKUNDA AKABIDHIWA VIFAA VYA KUKIMBILIA

    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, akikabidhiwa vifaa vya kukimbilia (Running Kit) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa ajili ya Kushiriki SUMAJKT Marathon itakayofanyika Tarehe 07 Juni 2026 (Jumapili hii) katika eneo la SUMAJKT House lililopo Medeli East jirani na Taa za Barabarani zilizopo njia panda ya kuelekea kwa Waziri Mkuu Jijini Dodoma. Kupata ratiba nzima ya Marathon gusa link hii hapa

  • Brig. Ngata awataka Wakurugenzi kuongeza Ubunifu

    Brig. Ngata awataka Wakurugenzi kuongeza Ubunifu. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewataka Wakurugenzi waendeshaji wa Viwanda vya Uzalishaji Maji, Ushonaji na Shule ya Sekondari Jitegemee vilivyopo Mgulani JKT kuongeza ubunifu katika Uendeshaji wa Miradi ya kiuchumi na yenye tija kwa Taifa. Brigedia Jenerali Ngata, amesema hayo Oktoba 03, 2025 alipotembelea viwanda pamoja na shule ya Jitegemee kwa lengo la kuona maendeleo ya viwanda hivyo vilivyopo mgulani JKT jijini Dar es Salaam. Aidha, Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema Makao Makuu ya Shirika inaendelea kuboresha Viwanda, Kampuni, Miradi na Shule…

  • |

    Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu

    Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu. Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu na Askari kutoka Jeshi la Uganda (UPDF) wakiongozwa na Meja Jenerali Willium Nabasa, leo tarehe 29 Aprili 2025 wametembelea Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es Salaam ili kujifunza shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa na SUMAJKT kwa manufaa ya kuliendeleza Jeshi la Uganda. Maafisa hao wamepokelewa na Mkuu wa Shule ya Jitegemee Kanali Emmanuel Mwaigobeko, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizungumzia ugeni huo Kanali Mwaigobeko, amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza Shughuli zinazofanywa na JKT pamoja na SUMAJKT. Jeshi la…

  • SUMAJKT Electric Co yafikisha umeme Gairo na Kilosa

    Kampuni ya Umeme ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT imekamilisha mradi wa Upelekaji Umeme katika Wilaya ya Gairo na Kilosa za Mkoa wa Morogoro. Mradi wa Upelekaji Umeme katika Vijiji hivyo ni Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita Kupitia wizara ya Nishati ambapo SUMAJKT Electric Co. Ltd. imeshirkiana vyema na Wakala wa Nishaji Vijiji REA katika kuhakikisha Umeme unafika kwa wakati. Katika wilaya ya Gairo idadi ya vijiji nane ambavyo ni Nongwe, mtega, Lukinga, Mkobwe, Mahelo,, Lufikili, Njungwa,Ikwamba tayari vimepata Umeme. Aidha katika wilaya ya Kilosa Vijiji vya Mfuluni na Idete navyo tayari vimepata…

  • WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CDF NA MAKAMANDA WA JWTZ KWA MWAKA 2024

    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, amefungua Mkutano wa Nane wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika Ukumbi wa Jenerali Jacob Mkunda uliopo katika Kikosi cha JKT Msange mkoani Tabora leo Desemba 16,2024 Mhe. Dkt. Stergomena Tax amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuendeleza utaratibu wa kufanya kikao hicho kikubwa Jeshini kwa Makamanda, kwani kinatoa fursa ya kutafakari na kushauriana masuala mbalimbali ya kiutendaji. Aidha, Mhe. Dkt. Stergomena Tax ameweza pia kuzindua Bwalo la Vijana wa JKT katika Kikosi hicho lililopewa…