Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electrical Co Ltd kuongezewa kandarasi za kusambaza umeme.

Kampuni ya Umeme ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Electrical Co Ltd. Imepongezwa kwa kutekeleza kwa wakati na weledi Mkubwa kandarasi ambazo imekua ikiingia mikataba.

Akizungumza Naibu waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko katika hafla ya kutia saini mkataba wa kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia katika makambi 22 ya JKT kwa mikoa 14 uliyosainiwa baina ya JKT na Wakala wa Nishati vijijini REA,Tukio lililofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko amelipongeza Shirika la Uzalishaji Mali la JKT(SUMA JKT) kupitia SUMAJKT Electric Co.Ltd kwa kukamilisha miradi ya kusambaza umeme vijijini haraka na kwa wakati husika.

“Katika Wakandarasi wanaotupa fahari sisi Wizara ya Nishati ni SUMA JKT chini ya Brigedia Jenerali Petro Ngata, miradi yao wamemaliza kwa haraka na kwa muda hivyo SUMA JKT wanastahili kupewa miradi mingine mingi kwa sababu usimamizi wa miradi yao wanayoifanya inatupa heshima sisi kama Serikali” alisema..Dkt.Biteko.

ameyasema hayo Septemba 13,2024 jijini Dodoma wakati akizindua jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa kuwezesha miradi ya nishati safi ya kupikia katika makambi 22 ya JKT kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

Aidha, Dkt.Biteko amesema kuwa wanakwenda kwenye miradi ya kupeleka umeme katika vitongoji mbalimbali hapa nchini, hivyo amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya REA pamoja na menejimenti, kuhakikisha kwamba kama kuna mahali panahitaji kazi ya dharura na ya haraka wapatiwe SUMA JKT.

Similar Posts

  • |

    KAMISHNA WA JKT KUTOKA NCHINI NAMIBIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA SUMAJKT

    Kamishna wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Namibia Dkt. Felix Masukubili amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Leo tarehe 18 Novemba 2024 Mlalakuwa Jijini Dar es Salaam. Dkt. Masukubili amepokelewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji Kanali Festus Mang’wela. Akiwa katika ziara hiyo amejionea shughuli za uzalishaji Mali zinazofanywa na SUMAJKT ikiwemo kiwanda cha kutengeneza Taa cha SUMAJKT SKYZONE CO.LTD ambacho kinazalisha taa zinazotumia nishati ya jua na umeme, kilichopo Mlalakuwa…

  • SUMAJKT, NYUMBU NA MZINGA KUENDELEZA USHIRIKIANO

    Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo. Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam. Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga….

  • Nyumba 2,500 zakamilika Msomera, Umeme asilimia 98, Miundombinu mbioni kukamilika

    Na Kassim Nyaki, Msomera Tanga. Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 21 Novemba, 2024 imefanya ziara ya kikazi kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro wanaoendelea kuhamia eneo hilo. Akiongoza bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) amezipongeza Sekta zote zinazohusika kutekeleza mradi huo kijiji cha Msomera kwa kukamilisha Nyumba 2500, ujenzi wa miundombinu ya Maji, mawasiliano, barabara, minada, majosho, kituo cha kuuzia maziwa, shule, zahanati, shule, kutenga maeneo ya malisho na miundombinu mingine kijijini hapo….

  • Waziri Kabudi aridhishwa na Ujenzi wa viwanja kwa ajili ya CHAN.

    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Palamagamba Kabudi (Mb) ameridhishwa na kazi inayofanywa na Kampuni ya SUMAJKT Construction Company Ltd, katika ujenzi wa viwanja vya mazoezi kwa ajili michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) yatakayofanyika mwezi Februari mwaka 2025. Katika Ukaguzi huo Profesa Kabudi, amefafanua kwamba viwanja hivyo vitakamilika ifikapo tarehe 21 Januari 2025 kwa ajili ya kuanza kutumika kwa mazoezi ya michuano ya CHAN. Nae Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, kwa niaba JWTZ ameeleza kwamba JKT limekabidhiwa kazi hivyo litaitekeleza kazi hiyo kwa muda uliopangwa….

  • |

    SUMAJKT Electric Co Ltd kuwasha umeme vijiji 51 wilayani Kishapu, Shinyanga.

    Zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme limefanyika Februari 17, 2023 wilayani Kishapu, katika Kijiji cha Itilima Shule ya Msingi Isunda, mkoani Shinyanga huku vijiji vitatu vikiwashiwa pia huduma ya umeme ambavyo ni Itilima, Ikonokelo na Ipeja. Mkandarasi SUMAJKT Electric Co Ltd ambaye anatekeleza mradi wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa Pili wilayani Kishapu na Shinyanga, ameanzakusambaza huduma za umeme katika Vijiji, Kaya na Taasisi za Serikali. Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme wilayani Kishapu kwa vijiji hivyo vitatu, amepongeza kasi ambayo SUMAJKT Electric Co Ltd wameanza nayo ya kusambaza…

  • Nyumba 5000 zakamilika Msomera

    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujemga Taifa SUMAJKT, Kupitia Kampuni ya Ujenzi ya @sumajktccl limekamilisha awamu ya Kwanza ya Mradi wa Nyumba 2500 katika Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Mkoani Tanga. Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji iliyotumika kukamilisha nyumba hizo. Taarifa zaidi tizama video hii hapa chini..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *