|

SUMAJKT Electric Co Ltd kuwasha umeme vijiji 51 wilayani Kishapu, Shinyanga.

Zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme limefanyika Februari 17, 2023 wilayani Kishapu, katika Kijiji cha Itilima Shule ya Msingi Isunda, mkoani Shinyanga huku vijiji vitatu vikiwashiwa pia huduma ya umeme ambavyo ni Itilima, Ikonokelo na Ipeja. Mkandarasi SUMAJKT Electric Co Ltd ambaye anatekeleza mradi wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa Pili wilayani Kishapu na Shinyanga, ameanzakusambaza huduma za umeme katika Vijiji, Kaya na Taasisi za Serikali.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme wilayani Kishapu kwa vijiji hivyo vitatu, amepongeza kasi ambayo SUMAJKT Electric Co Ltd wameanza nayo ya kusambaza umeme kwa wananchi na taasisi za Serikali, na kuwaomba waendelee na kasi hiyo hiyo ili kufikia Agosti mwaka huu vijiji vyote 51 wilayani humo viwe na huduma ya umeme.
“Shukrani SUMAJKT naomba muendelee na bidii ya kuunganisha umeme kwa wananchi na Taasisi za Serikali na ikifika Agosti vijiji vyote 51 wilayani Kishapu viwe na umeme na kuchochea maendeleo ya kiuchumi,” amesema Mkude.


“Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kutekelezwa miradi hii ya umeme vijijini ambacho kilikuwa kilio cha wananchi kwa muda mrefu lakini ndani ya utawala wake wa miaka miwili wananchi wa Kishapu wanapata umeme na leo tumewasha katika vijiji vitatu,” ameongeza Mkude.


Naye Meneja wa Shirika la ugavi wa umeme Tanzania mkoani Shinyanga (TANESCO) Mhandisi Leo Mwakatobe, amesema Shirika hilo litapeleka wataalam kwenye vijiji hivyo vilivyounganishiwa Nishati ya umeme ili kutoa elimu kwa wananchi na wajiunge kwa wingi kuunganishiwa huduma hiyo.


Meneja wa TANESCO wilayani Kishapu Mhandisi Elias Turnbull, amewaonya wananchi ambao tayari wana Nishati ya umeme kijijini kwao, wasije wakatumia vishoka kuunganisha umeme kwenye Kaya zao bali watumie wataalam kutoka TANESCO.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema amefurahishwa na kasi ya usambazaji umeme katika vijiji wilayani Kishapu, na kuwaomba wananchi wasihujumu mradi huo na kuiba miundombinu yake na kuiingiza hasara Serikali, huku akiwataka viongozi na Jeshi la Jadi Sungusungu kuhakikisha ulinzi unaimarika ili usifanyike wizi wowote wa vifaa.


Aidha, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya umeme kutoka SUMA JKT Major James Mhame, amesema kwa kasi waliyonayo ya kusambaza umeme vijijini wilayani Kishapu kwamba hadi kufikia Agosti mwaka huu vijiji vyote 51 vitakuwa na huduma ya Nishati ya umeme, pamoja na wilaya ya Shinyanga vijiji 50 ambapo huko kampuni ya SUMAJKT Electric Co Ltd tayari wameshawasha umeme
vijiji 10, Kishapu vijiji vitatu na wiki ijayo watawasha tena vijiji vingine.


“Kasi tuliyonayo ni nzuri tayari tumeshapokea nguzo za
umeme 400 na zinakuja tena zingine 6,000 tunamuahidi
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hatutamwangusha kwa
kutuamini sisi SUMAJKT na kutupatia kazi hii ya
kusambaza Nishati ya umeme vijijini na tutamaliza ndani
ya muda,”amesema Meja Mhame.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Itilima Mkwaya Mwandu, amesema kupata huduma hiyo ya Nishati ya umeme Kijijini humo itachochea fursa za kiuchumi, na kuipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi huo wa umeme wa REA vijijini.

Similar Posts

  • Waziri wa Ulinzi Angola apongeza malezi ya JKT kwa vijana

    Waziri wa Ulinzi wa Angola apongeza namna Jeshi la Kujenga Taifa linavyowalea Vijana wa Kitanzania. Waziri wa Ulinzi wa Angola Mhe.Joao Ernesto Das Santos ametoa pongezi hizo katika mwendelezo wa ziara yake hapa nchini, ambapo ametembelea Kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mkoa wa Pwani tarehe 9 Januari 2025.

  • Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta

    Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema shirika lina dhamira ya kuendelea kujitanua na kuimarisha miundombinu ya kimkakati ya biashara ikiwemo sekta ya nishati. Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema hayo katika uzinduzi wa gari la kusafirishia mafuta la Kampuni ya SUMAJKT Logistiki leo tarehe 26 Mei 2025, Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam. Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua gari hilo litaongeza ufanisi katika usambazaji wa nishati ya…

  • Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa

    Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amewataka Wakurugenzi Waendeshaji, Wakuu wa Shule na Miradi kutumia vizuri fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija kwa Shirika. Brigedia Jenerali Ngata ameyasema hayo tarehe 15 Agosti 2025 katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho Brigedia Jenerali Ngata amehimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Shirika. Aidha, amewasisitiza kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma katika…

  • SUMAJKT yazindua gari kuongeza ufanisi shule ya Kawawa

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa. Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla. Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari…

  • Brig. Ngata akagua maandalizi Gymkhana

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, tarehe 14 Novemba 2024 amekagua maandalizi ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu Gymkhana Dar es Salaam kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayofanyika mwaka 2027. Katika Ukaguzi huo Brigedia Jenerali Ngata, ameongozana na Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu Shirikisho la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) Salum Madadi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Mhandisi Morgan Nyonyi na Kapteni wa Gymkhana Football Club, Bw. Saleh Geva.

  • |

    Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi

    Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Daniel Sillo ayashauri mashirika ya Kijeshi ndani ya Nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Sayansi na Teknolojia katika uzalizalishaji wa bidhaa zao. Mhe. Sillo amesema hayo leo tarehe 25 Februari 2025 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mashirika yanayo milikiwa na  Majeshi ya  nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Geraffe iliyopo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi, Amefafanua kuwa Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Viwanda vilivyopo ndani ya Majeshi yaliyopo katika Jumuiya ya…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *