Dkt. Rhimo Nyansaho atembelea SUMAJKT MM
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (MB) leo tarehe 22, Julai 2026, ametembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na maendeleo yanayotekelezwa na shirika hilo. Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Nyansaho, alipata maelezo kuhusu miradi mbalimbali ya uzalishaji mali, mafanikio yaliyopatikana pamoja na mipango ya kuimarisha uwezo wa shirika katika kuchangia maendeleo ya taifa. Aidha, ziara hiyo ilihitimishwa kwa Mhe. Waziri Nyansaho, kutembelea kiwanda cha Maji ya Kunywa ya Uhuru Peak (SUMAJKT Bottling Co.Ltd) na Kiwanda cha Ushonaji nguo (SUMAJKT Garments Co….


