|

Dkt. Rhimo Nyansaho atembelea SUMAJKT MM

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (MB) leo tarehe 22, Julai 2026, ametembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na maendeleo yanayotekelezwa na shirika hilo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Nyansaho, alipata maelezo kuhusu miradi mbalimbali ya uzalishaji mali, mafanikio yaliyopatikana pamoja na mipango ya kuimarisha uwezo wa shirika katika kuchangia maendeleo ya taifa.

Aidha, ziara hiyo ilihitimishwa kwa Mhe. Waziri Nyansaho, kutembelea kiwanda cha Maji ya Kunywa ya Uhuru Peak (SUMAJKT Bottling Co.Ltd) na Kiwanda cha Ushonaji nguo (SUMAJKT Garments Co. Ltd) na kupongeza uongozi na watumishi wa shirika kwa juhudi zao na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo.

Katika ziara hiyo, Mhe Nyansaho aliongozana na Kamishna wa Mipango na Maendeleo Jeshini, Rear Admiral Mumanga na kupokelewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele akiongoza upande wa wenyeji akiwemo Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, Naibu Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Shule na Miradi SUMAJKT.

Similar Posts

  • Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane

    Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kuboresha Maonesho ya Wakulima Nanenane katika Banda la JKT. Dkt. Serera ametoa pongezi hizo leo tarehe 6 Agost 2025, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa Nzuguni Dodoma. Vilevile, Dkt. Serera amefurahishwa na Ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa na Huduma zinazotolewa na JKT pamoja na Shirika lake la SUMAJKT. Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa…

  • Waziri wa Ulinzi Comoro atembelea SUMAJKT Makao Makuu

    Waziri wa Ulinzi ambaye pia ni Katibu wa Rais nchini Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) ikiwa ni Mwendelezo wa Mazungumzo ya kushirikiana katika biashara baina ya Shirika Hilo na Comoro. Mhe. Yousoufa akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania – Comoro Khalfan Saleh amepokelewa na Kanali Robert Kessy kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata Makao Makuu Mlalakuwa Jijini Dar es salaam. Ikumbukwe, ziara hiyo ya Mhe. Yousoufa Mohamed Ali imetokana na Makubaliano ya Awali ya kibiashara kati ya SUMAJKT na…

  • Mej Jen. Isamuhyo (Mstaafu) aongoza kikao cha bodi SUMAJKT

    Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Michael Isamuhyo (mstaafu) ameongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri SUMAJKT na kufanya ziara ya kutembelea Viwanda vya Shirika ambavyo ni kiwanda cha Viatu na Bidhaa Ngozi, Kiwanda cha Insignia, Kiwanda cha Maji, Kiwanda cha Ushonaji pamoja na kituo cha mafuta SUMAJKT Energies. Ziara hiyo ya Bodi ya Ushauri SUMAJKT kutembelea viwanda imefanyika Machi 5, 2026 jijini Dar es Salaam. Aidha, ziara hiyo ni sehemu ya utambulisho wa shughuli zinazofanywa na Shirika kwa Bodi ya Ushauri Mpya iliyoanza kufanya kikao cha kwanza leo…

  • Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT

    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi…

  • GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana…

  • Brigedia Jenerali Petro Ngata apokelewa kwa Furaha SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa Brigedia Jenerali Petro Ngata, amepokelewa kwa furaha na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano, Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Brigedia Jenerali Ngata akipokelewa kwa mara ya kwanza tangu apandishwe cheo hicho kutoka cheo cha Kanali, alianza kukaribishwa kwa gwaride la heshima na baadae kupokelewa na kamati ya Utendaji ya SUMAJKT. Akizungumza katika ukumbi wa mikutano Brigedia Jenerali Ngata ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu Meja Jenerali Rajab Mabele…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *