• Suma Admin
    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema, kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa vihatarishi katika utendaji, Shirika limeamua kufanya mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watendaji ili kuwajengea uwezo katika kutambua, kutathimini na kudhibiti vihatarishi kwa lengo la kuleta tija katika utendaji. Brigedia Jenerali Ngata, amezungumza hayo Machi 4, 2026 katika ukumbi wa Umoja unaosimamiwa na SUMAJKT Catering Co.Ltd uliopo Mwenge Dar es Salaam.
  • Suma Admin
    Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz Twendezetu Pace ya Kwata Mapigano Na Mwendo
  • Suma Admin
    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, akikabidhiwa vifaa vya kukimbilia (Running Kit) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa ajili ya Kushiriki SUMAJKT Marathon itakayofanyika Tarehe 07 Juni 2026 (Jumapili hii) katika eneo la SUMAJKT House lililopo Medeli East jirani na Taa za Barabarani zilizopo njia panda ya kuelekea kwa Waziri Mkuu Jijini Dodoma. Kupata ratiba nzima ya Marathon gusa link hii hapa Ratiba 2 SUMAJKT Marathon – SUMAJKT MarathonDownload
  • Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (MB) leo tarehe 22, Julai 2026, ametembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na maendeleo yanayotekelezwa na shirika hilo. Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Nyansaho, alipata maelezo kuhusu miradi mbalimbali ya uzalishaji mali, mafanikio yaliyopatikana pamoja na mipango ya kuimarisha uwezo wa shirika katika kuchangia maendeleo ya taifa. Aidha, ziara hiyo ilihitimishwa kwa Mhe. Waziri Nyansaho, kutembelea kiwanda cha Maji ya Kunywa ya Uhuru Peak (SUMAJKT Bottling Co.Ltd) na Kiwanda cha Ushonaji nguo (SUMAJKT Garments Co.