-
Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo. Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam. Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga.
-
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Shija Lupi, ametembelea Eneo la Mauzo (Show room) la Kampuni ya Samani (SUMAJKT Chang’ombe Furniture Co.Ltd) lililopo karibu na Barabara ya Mwai kibaki Mlalakuwa Jijini Dar es salaam, tarehe 01 Disemba 2025 ili kuona Mwenendo wa biashara unavyoendelea. Brigedia Jenerali Lupi amepokelewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo Meja Hemed Mchwanga ambapo amemueleza kuwa Kasi ya wateja kununua Samani zinazozalishwa na Kampuni ya SUMAJKT imeongezeka mara dufu katika kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka. Kampuni ya Samani ya SUMAJKT imeendelea kuzalisha bidhaa Bora na
-
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi ya shirika hilo iliyomaliza muda wake kwa kuweka mbele Ubunifu, Mikakati pamoja na kuibua Miradi mipya ya kiuwekezaji. Mhe. Waziri Rhimo Nyansaho, amezungumza hayo leo tarehe 14 Januari 2026 baada ya kuzindua Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino jijini Dodoma. Aidha, Mhe. waziri Nyansaho amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kwao na kutoa rai kwao kuendelea kusaidia SUMAJKT kusonga mbele na kufikia malengo
-
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wa shirika kwa kuzalisha na kutoa huduma bora kupitia Kampuni tanzu za SUMAJKT. Brigedia Jenerali Ngata, ameongea hayo katika kikao cha tathimini cha shirika kilichofanyika Januari, 16, 2026 katika Ukumbi wa mkutano Makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Kanda za Ujenzi, Kampuni, Miradi na Shule.
-
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Michael Isamuhyo (mstaafu) ameongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri SUMAJKT na kufanya ziara ya kutembelea Viwanda vya Shirika ambavyo ni kiwanda cha Viatu na Bidhaa Ngozi, Kiwanda cha Insignia, Kiwanda cha Maji, Kiwanda cha Ushonaji pamoja na kituo cha mafuta SUMAJKT Energies. Ziara hiyo ya Bodi ya Ushauri SUMAJKT kutembelea viwanda imefanyika Machi 5, 2026 jijini Dar es Salaam. Aidha, ziara hiyo ni sehemu ya utambulisho wa shughuli zinazofanywa na Shirika kwa Bodi ya Ushauri Mpya iliyoanza kufanya kikao cha kwanza leo







