• Suma Admin
    Serikali kwa kupitia Wizara ya Michezo na Utamaduni imelikabidhi Shirika la Uzalishaji Mali za Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) Ujenzi wa Viwanja vya michezo idadi vitano. Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT amesema ujenzi wa viwanja hivyo utafanyika katika mtindo wa Operesheni ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya Muda uliowekwa. Taarifa zaidi, tizama video hii hapa chini:
  • Suma Admin
    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim atembelea SUMAJKT akiangalia Bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT. Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata akimpokea Gavana wa Ngazidja, Mze Mohamed Ibrahim alipowasili Makao Makuu ya SUMAJKT. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata alimpokea Gavana wa Ngazidja Mze Mohamed Ibrahim baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), tarehe 05 Octoba 2024. Ambapo Ugeni huo Ulikuja Tanzania kwa ajili ya Mahusiano ya kibiashara na SUMAJKT. Akiambatana na ujumbe kutoka Comoro, Gavana alipata
  • Suma Admin
    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana
  • Suma Admin
    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wote wa Umma JKT, wanaungana na familia kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT 2019-2021 Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu). Apumzike kwa Amani.
  • Suma Admin
    Habari zaidi tazama video hii hapa chini..