Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wote wa Umma JKT, wanaungana na familia kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT 2019-2021 Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu). Apumzike kwa Amani.
Similar Posts
SUMAJKT MARATHON YAZINDULIWA
Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz Twendezetu Pace ya Kwata Mapigano Na Mwendo
JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu waliobainika na watakaobainika kughushi vyeti
Jeshi la Kujenga Taifa JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu waliobainika na watakaobainika kughushi vyeti vya kuhitimu mafunzo. JKT imefikia uamuzi huo baada ya kubaini uwepo wa vyeti vya kughushi vilivyotumiwa na baadhi ya vijana ambao siyo waaminifu ili kujipatia ajira katika taasisi nakampuni zinazohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya jeshi hilo. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala, Kanali Juma Mrai amesema Jeshi la Kujenga Taifa lipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi na kampuni zote zinazohitaji uhakiki wa vyeti kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya JKT. JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu…
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aongoza waombolezaji kumuaga Meja Jenerali Charles Mbuge
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Octoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waomboleazaji, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tarehe 12 Octoba 2024. Miongoni mwa viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu…
CDF MKUNDA AKABIDHIWA VIFAA VYA KUKIMBILIA
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, akikabidhiwa vifaa vya kukimbilia (Running Kit) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa ajili ya Kushiriki SUMAJKT Marathon itakayofanyika Tarehe 07 Juni 2026 (Jumapili hii) katika eneo la SUMAJKT House lililopo Medeli East jirani na Taa za Barabarani zilizopo njia panda ya kuelekea kwa Waziri Mkuu Jijini Dodoma. Kupata ratiba nzima ya Marathon gusa link hii hapa
Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT amuaga Jenerali Musuguri
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es salaam. Tukio la Kuaga Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) aliyefariki Oktoba 29, 2024 limeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango. Viongozi wengine waliohudhuria Tukio hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Waziri wa Ulinzi Dkt. Stergomena Tax, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Maafisa Majenerali, Maafisa…


