• Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Octoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waomboleazaji, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tarehe 12 Octoba 2024. Miongoni mwa viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu
  • Suma Admin
    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) limeweka malengo ya kufikika na linaendelea kusimamia miradi kwa ufanisi ili kuleta tija kwa shirika. Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya (SUMAJKT) Meja Jenerali (mstaafu) Farah Mohamed, amesema hayo tarehe 19 Oktoba 2024 katika kikao cha kwanza cha malengo ya shirika cha mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa SUMAJKT Tower uliopo jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa wajumbe wa Bodi akiwemo Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata pamoja na wajumbe waalikwa
  • Suma Admin
    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Temeke Mhe. Jomary Satura, ameongoza wahitimu waliowahi kupata elimu yao katika shule ya SekondariJitegemee JKT, pamoja na wanachiwote kwenye zoezi la kufanya usafi katika soko la Temeke Sterio tarehe 2 Octoba 2024 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shule hio. Taarifa zaidi gusa video hii hapa chini..
  • Suma Admin
    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa. Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla. Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari
  • Suma Admin
    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujemga Taifa SUMAJKT, Kupitia Kampuni ya Ujenzi ya @sumajktccl limekamilisha awamu ya Kwanza ya Mradi wa Nyumba 2500 katika Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Mkoani Tanga. Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji iliyotumika kukamilisha nyumba hizo. Taarifa zaidi tizama video hii hapa chini..