• Suma Admin
    Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Oparesheni Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Michael Muhona ameipongeza Shule ya Sekondari Jitegemee JKT kwa kutimiza Miaka 50 Tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza katika Sherehe ya Maadhimisho hayo zilizoambatana na Harambee maalaumu ya kuchangia maboresho ya Shule hiyo Meja Jenerali Muhona amesema JWTZ linaunga mkono dhamira ya Mageuzi inayofanyika, huku akitoa wito kwa walimu kuhakikisha Shule inaendeleza viwango bora vya Ufahulu. Kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Jitegemee JKT kilifanyika tarehe 01 Novemba 2024 ukumbi wa Isamuhyo Mgulani JKT. CHANGIA ELIMU KWA MABORESHO YA MIUNDO MBINU1.NMB….236100419222.CRDB…01508929587003.LIPA….22426113 TIGO.4.LIPA….54359412 VODACOMMajina
  • Suma Admin
    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es salaam. Tukio la Kuaga Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) aliyefariki Oktoba 29, 2024 limeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango. Viongozi wengine waliohudhuria Tukio hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Waziri wa Ulinzi Dkt. Stergomena Tax, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Maafisa Majenerali, Maafisa
  • Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi ambaye pia ni Katibu wa Rais nchini Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) ikiwa ni Mwendelezo wa Mazungumzo ya kushirikiana katika biashara baina ya Shirika Hilo na Comoro. Mhe. Yousoufa akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania – Comoro Khalfan Saleh amepokelewa na Kanali Robert Kessy kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata Makao Makuu Mlalakuwa Jijini Dar es salaam. Ikumbukwe, ziara hiyo ya Mhe. Yousoufa Mohamed Ali imetokana na Makubaliano ya Awali ya kibiashara kati ya SUMAJKT na
  • Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Oppah Kashiri, amefanya ziara Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mlalakuwa Dar es salaam. Katika Ziara hiyo Mhe. Waziri Kashiri, akiwa na Waziri wa Ulinzi na JKT wa Tanzania Dkt. Stergomena Tax, alipatiwa taarifa ya shirika na kutembelea kiwanda cha Taa cha SUMAJKT Skyzone Co Ltd. Kilichopo Mlalakuwa na kiwamda cha Maji ya Kunywa cha SUMAJKT Bottling Co Ltd. Kilichopo Mgulani JKT.
  • Suma Admin
    Timu ya Mpira wa Miguu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT, imewasili Jijini Tanga hi tarehe 10 Novemba 2024, kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMMUTA) iliyoanza Kutimua vumbi katika jiji hilo. Akizungumza mara baada ya kuwasili Jijini Tanga Katibu wa Kamati ya SHIMMUTA Kapteni Kichawele Bokassa, amesema timu imejiandaa vizuri kushiriki Michuano hiyo.