• Suma Admin
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Albert Chalamila ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zilizopo Dar es Salaam kuhakikisha wanafika kiwanda cha SUMAJKT Skyzone kilichopo Mlalakua jijini hapo ili kutoa oda za kutengeneza taa bora za barabarani. “Tumepita tumeona teknolojia ya kiwanda hiki., naomba nitoe neno rasmi.., wakurugenzi wote wa halmashauri za Dar es Salaam, kufanya ziara mara moja katika kiwanda hiki, na ikiwezekana kutoa oda za taa.., ili ziweze kufungwa kwenye mji wetu kuhakikisha mji unafanya kazi masaa 24.” Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema kwamba Kiwanda hiko ni cha kwanza kabisa kwa aina
  • Suma Admin
    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, tarehe 14 Novemba 2024 amekagua maandalizi ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu Gymkhana Dar es Salaam kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayofanyika mwaka 2027. Katika Ukaguzi huo Brigedia Jenerali Ngata, ameongozana na Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu Shirikisho la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) Salum Madadi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Mhandisi Morgan Nyonyi na Kapteni wa Gymkhana Football Club, Bw. Saleh Geva.
  • Suma Admin
    Kamishna wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Namibia Dkt. Felix Masukubili amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Leo tarehe 18 Novemba 2024 Mlalakuwa Jijini Dar es Salaam. Dkt. Masukubili amepokelewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji Kanali Festus Mang’wela. Akiwa katika ziara hiyo amejionea shughuli za uzalishaji Mali zinazofanywa na SUMAJKT ikiwemo kiwanda cha kutengeneza Taa cha SUMAJKT SKYZONE CO.LTD ambacho kinazalisha taa zinazotumia nishati ya jua na umeme, kilichopo Mlalakuwa
  • Suma Admin
    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua magari matano yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni moja ya Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) Kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizindua magari hayo Leo tarehe 19 Novemba 2024, Brigedia Jenerali Petro Ngata ameeleza kuwa Menejimenti ya SUMAJKT imejiwekea mikakati ya kuendelea kuongeza vitendeakazi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT, Kapteni Rosemary
  • Suma Admin
    Na Kassim Nyaki, Msomera Tanga. Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 21 Novemba, 2024 imefanya ziara ya kikazi kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro wanaoendelea kuhamia eneo hilo. Akiongoza bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) amezipongeza Sekta zote zinazohusika kutekeleza mradi huo kijiji cha Msomera kwa kukamilisha Nyumba 2500, ujenzi wa miundombinu ya Maji, mawasiliano, barabara, minada, majosho, kituo cha kuuzia maziwa, shule, zahanati, shule, kutenga maeneo ya malisho na miundombinu mingine kijijini hapo.