-
Brigedia Jenerali George Itang’are alivyomuwakilisha Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT kupokea Ugeni wa Wakufunzi na Wanafunzi kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa Nchini Kenya. Taarifa zaidi tazama video hii hapa chini..
-
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, amefungua Mkutano wa Nane wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika Ukumbi wa Jenerali Jacob Mkunda uliopo katika Kikosi cha JKT Msange mkoani Tabora leo Desemba 16,2024 Mhe. Dkt. Stergomena Tax amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuendeleza utaratibu wa kufanya kikao hicho kikubwa Jeshini kwa Makamanda, kwani kinatoa fursa ya kutafakari na kushauriana masuala mbalimbali ya kiutendaji. Aidha, Mhe. Dkt. Stergomena Tax ameweza pia kuzindua Bwalo la Vijana wa JKT katika Kikosi hicho lililopewa
-
Waziri Wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Mhe. Stargomena Lawrence Tax, ameongoza Maafisa, Askari, Vijana, Watumishi wa Umma na Waombolezaji katika Mazishi ya Mwili Wa Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika katika Kijiji Cha Luchelele Jijini Mwanza tarehe 28 Desemba 2024. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, katika Mazishi hayo Mkuu wa Jeshi La Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema Marehemu Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) enzi za uhai wake akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ametumikia Jeshi kwa kipindi
-
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Palamagamba Kabudi (Mb) ameridhishwa na kazi inayofanywa na Kampuni ya SUMAJKT Construction Company Ltd, katika ujenzi wa viwanja vya mazoezi kwa ajili michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) yatakayofanyika mwezi Februari mwaka 2025. Katika Ukaguzi huo Profesa Kabudi, amefafanua kwamba viwanja hivyo vitakamilika ifikapo tarehe 21 Januari 2025 kwa ajili ya kuanza kutumika kwa mazoezi ya michuano ya CHAN. Nae Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, kwa niaba JWTZ ameeleza kwamba JKT limekabidhiwa kazi hivyo litaitekeleza kazi hiyo kwa muda uliopangwa.







