• Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi wa Angola apongeza namna Jeshi la Kujenga Taifa linavyowalea Vijana wa Kitanzania. Waziri wa Ulinzi wa Angola Mhe.Joao Ernesto Das Santos ametoa pongezi hizo katika mwendelezo wa ziara yake hapa nchini, ambapo ametembelea Kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mkoa wa Pwani tarehe 9 Januari 2025.
  • Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameridhishwa na shughuli zinazofanywa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT). Akizungumza baada ya kufanya ziara SUMAJKT leo tarehe 11 Januari 2025, Mhe. Dos Santos, amebainisha kuwa amevutiwa na uzalishaji unaofanywa na Shirika hilo, hivyo wataenda kufanyiakazi nchini kwao. “Wizara yetu ya Ulinzi nchini Angola kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania tutakuja kusaini hati ya awali ya makubaliano ambayo itaonesha maeneo ya kushirikiana” alisema Mhe. Dos Santos. Aidha, Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania kupitia JWTZ kwa kuwezesha
  • Suma Admin
    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa kutekeleza majukumu yake Meja Jenerali Mabele ametoa shukrani hizo tarehe 16 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT wakati wa hafla ya uzinduzi wa Magari aina ya Isuzu D Max Pick Up idadi tisa (9) kwaajili ya Matumizi ya shughuli za kiutawala ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa. Magari hayo yamekabidhiwa kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Makao Makuu ya JKT na Makamanda Vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa.
  • Suma Admin
    Kampuni ya Umeme ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT imekamilisha mradi wa Upelekaji Umeme katika Wilaya ya Gairo na Kilosa za Mkoa wa Morogoro. Mradi wa Upelekaji Umeme katika Vijiji hivyo ni Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita Kupitia wizara ya Nishati ambapo SUMAJKT Electric Co. Ltd. imeshirkiana vyema na Wakala wa Nishaji Vijiji REA katika kuhakikisha Umeme unafika kwa wakati. Katika wilaya ya Gairo idadi ya vijiji nane ambavyo ni Nongwe, mtega, Lukinga, Mkobwe, Mahelo,, Lufikili, Njungwa,Ikwamba tayari vimepata Umeme. Aidha katika wilaya ya Kilosa Vijiji vya Mfuluni na Idete navyo tayari vimepata
  • Suma Admin
    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameukaribisha Makao Makuu ya JKT Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ili kufanya mazungumzo ya namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo ndani Jeshi la Kujenga Taifa. Meja Jenerali Mabele ametoa ukaribisho huo leo tarehe 31 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, baada ya kufanyika kikao cha Utekelezaji wa Makubaliano kati ya JKT na SUA juu ya Mpango wa Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo hicho. Nae Dkt. Nyambelila Amouri kutoka RASI NDAKI ya Kilimo SUA mkoani Morogoro amesema, kupitia kikao hicho na ushirikiano uliopo