-
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 31 Januari 2025, amewaongoza Maafisa, Askari, Vijana na Watumishi wa Umma katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo pamoja na eneo la viwanja vya makazi ya watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Chinangali 2 nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema zoezi hilo ni muendelezo wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Samia
-
Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd imetia Saini Mkataba wa kufanya Usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Katika Maeneo ya Soko la Buguruni Pamoja na Soko la Ilala leo tarehe18 Februari 2025. Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Elihuruma Mabelya, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto, Madiwani, na wadau wa Maendeleo imehusisha pia Uzinduzi wa Magari yaliyo nunuliwa na jiji yatakayotumika Katika Usafi. Akizungumza mara baada ya Kutia Saini Mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Jonas Mpogolo,
-
Wataalamu wa Utafiti na Ushauri wa Kilimo kutoka Kampuni ya CAMPO nchini Brazil wametembelea Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation lililopo Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro kuanzia tarehe 11 Februari 2025. Wawakilishi wa kampuni ya CAMPO ambao ni Prof Jamil Macedo ambaye ni Mtalaam wa Udongo pamoja na Bwana Cezar Rizzi Mtalaam wa Umwagiliaji wamewasili Nchini Tanzania Tarehe 10 Februari 2025 na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, Kisha ugeni huo kuelekea Morogoro kutembelea Shamba ambalo awali liliitwa Kilombero Plantation Company Limited (KPL) na sasa SUMAJKT Mngeta Plantation kwa lengo la kufanya utafiti na kutoa ushauri wa
-
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Brigedia Jenerali Petro Ngata Ameitaka Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electric Co Ltd kuvitunza vitendea kazi vinavyonunuliwa ili viweze kudumu na kuleta tija kwa Shirika. Amezungumza hayo Tarehe 14 Februari 2025, baada ya  kufanya Uzinduzi wa Gari Jipya la utawala lililonunuliwa na Kampuni hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi. Awali akitoa taarifa fupi ya ununuzi wa gari hilo Mkurugenzi Mwendeshaji wa SUMAJKT Electric Co Ltd. Meja James Mhame, amesema kuongezeka kwa gari hilo kutarahisisha utekelezaji wa majukumu yao. SUMAJKT Electric Co.Ltd  Inajishughulisha na Kandarasi mbalimbali za Miundombinu
-
Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Daniel Sillo ayashauri mashirika ya Kijeshi ndani ya Nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Sayansi na Teknolojia katika uzalizalishaji wa bidhaa zao. Mhe. Sillo amesema hayo leo tarehe 25 Februari 2025 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mashirika yanayo milikiwa na Majeshi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Geraffe iliyopo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi, Amefafanua kuwa Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Viwanda vilivyopo ndani ya Majeshi yaliyopo katika Jumuiya ya







