Wataalamu wa Utafiti na Ushauri wa Kilimo kutoka Kampuni ya CAMPO nchini Brazil wametembelea Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation
Wataalamu wa Utafiti na Ushauri wa Kilimo kutoka Kampuni ya CAMPO nchini Brazil wametembelea Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation lililopo Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro kuanzia tarehe 11 Februari 2025. Wawakilishi wa kampuni ya CAMPO ambao ni Prof Jamil Macedo ambaye ni Mtalaam wa Udongo pamoja na Bwana Cezar Rizzi Mtalaam wa Umwagiliaji wamewasili Nchini Tanzania Tarehe 10 Februari 2025 na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, Kisha ugeni huo kuelekea Morogoro kutembelea Shamba ambalo awali liliitwa Kilombero Plantation Company Limited (KPL) na sasa SUMAJKT Mngeta Plantation kwa lengo la kufanya utafiti na kutoa ushauri wa…


