• Suma Admin
    Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda. Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, amefunga Kikao cha Wakuu wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo tarehe 26 Feb 2025  katika hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Salum Othman, amesema Mkutano huo huibua fursa, Masoko  na namna nzuri ya kuboresha teknolojia  ya Viwanda na Mashirika ya jumuiya hiyo. Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda. Akizungumza kuhusu lengo la Mkutano huo, ameeleza ni kuweka pamoja  na kuimarisha ushirikiano wa Mashirika
  • Suma Admin
    ” KUSITISHWA KWA MAFUNZO YA JKT KULILETA ATHARI KUBWA IKIWEMO YA MMOMONYOKO WA MAADILI”Wakuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (Wastaafu)Meja Jenerali Martin Madata (Mstaafu) na Meja Jenerali Samwel Kitundu (Mstaafu), wakielezea umuhimu wa Mafunzo ya JKT, athari zilizopatikana baada ya kusitishwa kwa Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na Kujitolea pamoja na Mafanikio yaliyopatikana Baada ya kurejeshwa kwa Mafunzo hayo. Wameyasema hayo wakati wa Mahojiano Maalumu ya Mafanikio yaliyopatikana ndani ya JKT kwa kipindi cha Miaka 60 ya Uwepo wake nchini.https://www.instagram.com/reel/DGvnVdetkhE/?igsh=ZmJua2s1NWlvcndw Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
  • Suma Admin
    Ugeni wa Wakufunzi na Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa nchini Nigeria (NDC) Wafanya ziara ya Kimasomo Katika Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mlalakuwa Dar es salaam, leo tarehe 04 Machi 2025 kwa lengo la kujifunza namna Shirika linavyofanya Shughuli za Uzalishaji wa Bidhaa hususani Viwandani. Ugeni huo wa Wakufunzi na wanafunzi idadi 26 ukiongozwa na Mkuu wa Msafara ‘ Air Vice Marshal’ Hanidu Ibrahim, umepokelewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu
  • Suma Admin
    Washiriki wa Kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Mataifa 16 Duniani wamefanya ziara ya Kimafunzo Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma mnamo Machi 10, 2025. Wakiwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamepata wasilisho la Namna JKT na Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) linavyotekeleza majukumu yake ya Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali na Ulinzi. https://www.instagram.com/p/DHBmQZOIPxl/?igsh=cXZmNjdhZGp1ZDFw Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
  • Suma Admin
    Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imefanya ziara kutembelea ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Dodoma leo tarehe 12 Machi 2025 na kupongeza mafanikio yaliyofikiwa. Akizungumza kwa niaba ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Namtumbo Mheshimiwa Vita Kawawa amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman kwa mafanikio makubwa ya ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa. Kamati hiyo imelipongeza JWTZ kwa kukidhi vigezo vya ujenzi, ubora wa