• Suma Admin
    Jeshi la Kujenga Taifa JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu waliobainika na watakaobainika kughushi vyeti vya kuhitimu mafunzo. JKT imefikia uamuzi huo baada ya kubaini uwepo wa vyeti vya kughushi vilivyotumiwa na baadhi ya vijana ambao siyo waaminifu ili kujipatia ajira katika taasisi nakampuni zinazohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya jeshi hilo. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala, Kanali Juma Mrai amesema Jeshi la Kujenga Taifa lipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi na kampuni zote zinazohitaji uhakiki wa vyeti kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya JKT. JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu
  • Suma Admin
    Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), aongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika leo tarehe 14 Machi 2025 katika ukumbi wa Mebele jijini Dodoma. Lengo la kikao hicho ni mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kupitisha makadirio ya bajeti ijayo ya mwaka wa fedha wa 2025/2026. Kikao hicho cha Bodi ya Ushauri SUMAJKT kimehudhuriwa na Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele,
  • Suma Admin
    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi
  • Suma Admin
    Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana. Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amewaasa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutekeleza kwa weledi jukumu la Malezi ya Vijana. Kanali Mrai ametoa rai hiyo tarehe 21 Machi 2025 wakati akihitimisha Semina Elekezi ya Maafisa wa JWTZ waliopewa Uhamisho kwenda JKT, iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiendesha Semina Elekezi kwa watendaji wake ili kuwajengea uwezo wa
  • Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax ameupongeza uongozi wa kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mkoani Pwani kwa kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati ya gesi kwa asilimia 100. Ruvu JKT waachana na matumizi ya kuni na mkaa. Mhe.Dkt. Tax ametoa pongezi hizo tarehe 3 Aprili 2025 wakati alipofanya ziara kikosini hapo na kujionea namna kikosi hicho chini ya Uongozi wa kamanda kikosi Kanali Peter Mnyani unavyotekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa Taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100. Waziri wa Ulinzi