• Suma Admin
    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ, kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo sasa wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpira wa magongo na mpira wa kikapu. “Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi
  • Suma Admin
    Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Mhe. Williman Kapenjama, amewaasa na kuwakumbusha vijana wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi kundi la Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano juu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii. Vijana wahitimu waaswa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mhe. Kapenjama, amezungumza hayo leo tarehe 08 Aprili 2025, alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kundi la kujitolea katika kikosi mlale JKT mkoani Ruvuma. Aidha, amebainisha kuwa vijana wengi hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hivyo hutazama mambo ambayo ni kinyume na tamaduni za kiafrika. Nae Mwakilishi
  • Suma Admin
    Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT. Mkuu wa Tawi la Mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Longinus Nyingo tarehe 16 Aprili 2025 amekagua Maandalizi ya Mwisho kuelekea kuhitimishwa kwa zoezi la Ufungaji wa Mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano katika Kikosi cha Ruvu JKT Mlandizi mkoani Pwani. Kanali Nyingo amesema kuwa, zoezi la ufungaji wa Mafunzo katika Vikosi vyote vya JKT lilianza tarehe 8 Aprili 2025 ambapo Mkuu wa JKT alikuwa akiwakilishwa na Wakuu wa Matawi
  • Suma Admin
    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza mafunzo ya vijana wa JKT. Mkuu wa JKT amshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu mafunzo ya JKT. Meja Jenerali Mabele, ameyasema hayo leo tarehe 17 Aprili 2025 alipokuwa anahitimisha mafunzo ya Awali ya kijeshi kwa vijana wa Operesheni miaka 60 ya Muungano katika kikosi Cha Ruvu JKT kilichopo mlandizi mkoani Pwani. Amesema Malezi ni suala Mtambuka, yanaanzia ngazi ya familia, Vijana wanapofika makambini.
  • Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali John Jacob Mkunda akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa Kampuni ya SUMAJKT Life Insurance, zilizofanyika katika Ukumbi wa Super Dome jijini Dar es Salaam.
    Suma Admin
    Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amepokea ugeni wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka nchini Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi, ambaye amefanya ziara Makao Makuu ya SUMAJKT ili kubadilishana uzoefu katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo. Ugeni huo baaba ya kupokelewa leo tarehe 28 Aprili 2025 umetembelea Kiwanda cha SUMAJKT Skyzon Co. Ltd, Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi na Mradi wa SUMAJKT Energies ili kujionea shughuli za