Ugeni wa Wakufunzi na Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa nchini Nigeria (NDC) Wafanya ziara ya Kimasomo Katika Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT)

Ugeni wa Wakufunzi na Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa nchini Nigeria (NDC) Wafanya ziara ya Kimasomo Katika Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mlalakuwa Dar es salaam, leo tarehe 04 Machi 2025 kwa lengo la kujifunza namna Shirika linavyofanya Shughuli za Uzalishaji wa Bidhaa hususani Viwandani.

Ugeni huo wa Wakufunzi na wanafunzi idadi 26 ukiongozwa na Mkuu wa Msafara ‘ Air Vice Marshal’ Hanidu Ibrahim, umepokelewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele.

Akizungumza baada ya Ziara hiyo, ‘Air Vice Marshal’ Ibrahim amebainisha wamehamasika na uzalishaji unaofanywa na SUMAJKT kupitia kiwanda cha Taa, Maji, Ushonaji Nguo na Bidhaa za Ngozi.

“Lengo la ziara yetu ni Kujifunza Shughuli zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake SUMAJKT na namna linavyochangia katika Uchumi wa Tanzania, hivyo tumejifunza Mengi tutaenda kuyatumia katika Kujenga Uchumi wa Taifa letu Nigeria” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Kanali Shija Lupi amesema Ugeni huo umeridhishwa na kazi za SUMAJKT.

Ugeni huo umepata fursa ya kutembelea Kiwanda cha Taa (SUMAJKT Skyzon Co.Ltd), Kiwanda cha Maji (SUMAJKT Bottling Co.Ltd), Kiwanda cha Ushonaji Nguo (SUMAJKT Garments Co.Ltd) na Bidhaa za Ngozi.

Similar Posts

  • DED SUMAJKT atembelea Mafinga.

    DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa. Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi. Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea…

  • GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana…

  • SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

    SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…

  • |

    Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu

    Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu. Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu na Askari kutoka Jeshi la Uganda (UPDF) wakiongozwa na Meja Jenerali Willium Nabasa, leo tarehe 29 Aprili 2025 wametembelea Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es Salaam ili kujifunza shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa na SUMAJKT kwa manufaa ya kuliendeleza Jeshi la Uganda. Maafisa hao wamepokelewa na Mkuu wa Shule ya Jitegemee Kanali Emmanuel Mwaigobeko, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizungumzia ugeni huo Kanali Mwaigobeko, amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza Shughuli zinazofanywa na JKT pamoja na SUMAJKT. Jeshi la…

  • Timu ya Mpira wa Miguu SUMAJKT yawasili Tanga kushiriki SHIMMUTA

    Timu ya Mpira wa Miguu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT, imewasili Jijini Tanga hi tarehe 10 Novemba 2024, kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMMUTA) iliyoanza Kutimua vumbi katika jiji hilo. Akizungumza mara baada ya kuwasili Jijini Tanga Katibu wa Kamati ya SHIMMUTA Kapteni Kichawele Bokassa, amesema timu imejiandaa vizuri kushiriki Michuano hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *