Shule ya Jitegemee JKT yatimiza miaka 50, Jenerali Mhona atia neno

Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Oparesheni Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Michael Muhona ameipongeza Shule ya Sekondari Jitegemee JKT kwa kutimiza Miaka 50 Tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza katika Sherehe ya Maadhimisho hayo zilizoambatana na Harambee maalaumu ya kuchangia maboresho ya Shule hiyo Meja Jenerali Muhona amesema JWTZ linaunga mkono dhamira ya Mageuzi inayofanyika, huku akitoa wito kwa walimu kuhakikisha Shule inaendeleza viwango bora vya Ufahulu.

Kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Jitegemee JKT kilifanyika tarehe 01 Novemba 2024 ukumbi wa Isamuhyo Mgulani JKT.

CHANGIA ELIMU KWA MABORESHO YA MIUNDO MBINU
1.NMB….23610041922
2.CRDB…0150892958700
3.LIPA….22426113 TIGO.
4.LIPA….54359412 VODACOM
Majina ya akaunti zote ni “JITEGEMEE (JKT) SECONDARY SCHOOL “

Mawasiliano:
+255755874191
+255717286100

Taarifa zaidi tumekuwekea kwenye chaneli yetu ya Youtube hapa chini..

Similar Posts

  • Kampuni ya usafi SUMAJKT yasaini mkataba na Halmashauri ya Jiji Dar

    Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd  imetia Saini Mkataba wa kufanya Usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Katika Maeneo ya Soko la Buguruni Pamoja na Soko la Ilala leo tarehe18 Februari 2025. Hafla hiyo ambayo  imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Elihuruma Mabelya, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto, Madiwani, na wadau wa Maendeleo imehusisha pia Uzinduzi wa Magari yaliyo nunuliwa na jiji yatakayotumika Katika Usafi. Akizungumza mara baada ya Kutia Saini Mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Jonas Mpogolo,…

  • VIJANA WAHITIMU JKT WAASWA MATUMIZI MAZURI YA MITANDAO YA KIJAMII

    Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Mhe. Williman Kapenjama, amewaasa na kuwakumbusha vijana wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi kundi la Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano juu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii. Vijana wahitimu waaswa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mhe. Kapenjama, amezungumza hayo leo tarehe 08 Aprili 2025, alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kundi la kujitolea katika kikosi mlale JKT mkoani Ruvuma. Aidha, amebainisha kuwa vijana wengi hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hivyo hutazama mambo ambayo ni kinyume na tamaduni za kiafrika. Nae Mwakilishi…

  • GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana…

  • SUMAJKT LAJIWEKEA MALENGO MWAKA WA FEDHA 2024/’25

    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) limeweka malengo ya kufikika na linaendelea kusimamia miradi kwa ufanisi ili kuleta tija kwa shirika. Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya (SUMAJKT) Meja Jenerali (mstaafu) Farah Mohamed, amesema hayo tarehe 19 Oktoba 2024 katika kikao cha kwanza cha malengo ya shirika cha mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa SUMAJKT Tower uliopo jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa wajumbe wa Bodi akiwemo Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata pamoja na wajumbe waalikwa…

  • Mwenyekiti kamati ya NaneNane akaribisha wananchi Dodoma

    Mwenyekiti kamati ya NaneNane akaribisha wananchi Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wakulima Nanenane Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Shija Lupi amewakaribisha wananchi wote hapa nchini kutembelea Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma na Kikanda katika Kanda zote ambazo Jeshi hilo linashiriki.

  • Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT

    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *