SUMAJKT yazindua gari kuongeza ufanisi shule ya Kawawa

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa.

Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla.

Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari hilo.

Uzinduzi wa Gari hilo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba 2024, Makao Makuu ya SUMAJKT na kuhudhuriwa na Maafisa Wakuu, Maafisa wadogo, Askari, Vijana watumishi wa Umma.

Kwa habari zaidi gusa video hapa chini..

Similar Posts

  • Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane

    Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kuboresha Maonesho ya Wakulima Nanenane katika Banda la JKT. Dkt. Serera ametoa pongezi hizo leo tarehe 6 Agost 2025, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa Nzuguni Dodoma. Vilevile, Dkt. Serera amefurahishwa na Ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa na Huduma zinazotolewa na JKT pamoja na Shirika lake la SUMAJKT. Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa…

  • SUMAJKT LAJIWEKEA MALENGO MWAKA WA FEDHA 2024/’25

    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) limeweka malengo ya kufikika na linaendelea kusimamia miradi kwa ufanisi ili kuleta tija kwa shirika. Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya (SUMAJKT) Meja Jenerali (mstaafu) Farah Mohamed, amesema hayo tarehe 19 Oktoba 2024 katika kikao cha kwanza cha malengo ya shirika cha mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa SUMAJKT Tower uliopo jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa wajumbe wa Bodi akiwemo Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata pamoja na wajumbe waalikwa…

  • Shule ya Jitegemee JKT yatimiza miaka 50, Jenerali Mhona atia neno

    Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Oparesheni Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Michael Muhona ameipongeza Shule ya Sekondari Jitegemee JKT kwa kutimiza Miaka 50 Tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza katika Sherehe ya Maadhimisho hayo zilizoambatana na Harambee maalaumu ya kuchangia maboresho ya Shule hiyo Meja Jenerali Muhona amesema JWTZ linaunga mkono dhamira ya Mageuzi inayofanyika, huku akitoa wito kwa walimu kuhakikisha Shule inaendeleza viwango bora vya Ufahulu. Kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Jitegemee JKT kilifanyika tarehe 01 Novemba 2024 ukumbi wa Isamuhyo Mgulani JKT. CHANGIA ELIMU KWA MABORESHO YA MIUNDO MBINU1.NMB….236100419222.CRDB…01508929587003.LIPA….22426113 TIGO.4.LIPA….54359412 VODACOMMajina…

  • SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

    SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…

  • CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya.

    CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob John Mkunda, amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa maono ya kuanzisha Kampuni ya Bima ya Maisha (SUMAJKT Life Insurance Co. Ltd) itakayokuwa Msaada mkubwa kwa Watanzania kwa Vizazi vya sasa na Vijavyo. Jenerali Mkunda, ameyasema hayo Tarehe 10 Mei 2025 katika Sherehe ya Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Maisha ya SUMAJKT tukio lililofanyika Ukunbi wa (The Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam. CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Amesema imani yake ni kuona watanzania wakipatiwa huduma hiyo ya Bima kwani Jeshi…

  • Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT

    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *