Brigedia Jenerali Petro Ngata apokelewa kwa Furaha SUMAJKT
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa Brigedia Jenerali Petro Ngata, amepokelewa kwa furaha na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano, Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Brigedia Jenerali Ngata akipokelewa kwa mara ya kwanza tangu apandishwe cheo hicho kutoka cheo cha Kanali, alianza kukaribishwa kwa gwaride la heshima na baadae kupokelewa na kamati ya Utendaji ya SUMAJKT. Akizungumza katika ukumbi wa mikutano Brigedia Jenerali Ngata ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu Meja Jenerali Rajab Mabele…


