-
-
BRIGEDIA JENERALI NGATA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYABIASHARA NCHINI COMORO
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi ka Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amefanya mazungumzo na Jumuiya ya wafanyabiashara kisiwani Comoro katika ukumbi wa Chambre de Commerce Ngazidja uliopo kisiwani humo. Kikao hicho kimefanyika tarehe 5 Septemba 2024, na wafanyabiashara wanaochukua bidhaa Tanzania na kuzipeleka nchini Comoro, Brigedia Jenerali Ngata alipata fursa ya kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT hususani katika Sekta ya Ujenzi, Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata ameeleza nia thabiti ya SUMAJKT kuhitaji kufanya kazi na wafanyabiashara hao katika nyanja ya Ujenzi na Kilimo. Kwa upande wa wafanyabiashara kisiwani Comoro wamesema…
-
SUMAJKT Kutafuta Fursa za Biashara visiwani Comoro
Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi. Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata. Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha…
-
SUMAJKT yashinda Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Nane Nane
SUMAJKT yashinda Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane). Tuzo hio imekabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Mabele. Meja Jenarali Mabele amesema siri ya ushindi wa JKT katika maonesho mbalimbali nchini ni dhamira ya kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa. Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo katika sherehe za Kilele cha Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane ambayo kitaifa yameadhimisha Jijini Dodoma na Kufungwa na Mh. Rais wa…
-
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akabidhi Tuzo kwa SUMAJKT
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amkabidhi tuzo ya Mshidi wa Jumla Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT katika sherehe za kufunga Mashindano ya #cdfcup2024 yaliyofanyika katika Uwanja wa uhuru, jijini Dar es salaam.


