JENERALI MKUNDA AZINDUA MITAMBO YA MAJI SUMAJKT BOTTLING CO. LTD, AFURAHISHWA NA JITIHADA ZA SHIRIKA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 16 Oktoba 2023 amezindua mitambo ya kuzalisha Maji ya kunywa ya Uhuru Peak katika kiwanda cha SUMAJKT Bottling Co. Limited kilichopo Mgulani JKT Jijini Dar es salaam.

Mitambo hiyo yenye thamani ya Tsh Bilioni Moja na milioni 800 inaanza kutumika rasmi kuanzia sasa ili kuongeza ufanisi wa kiwanda ikiwa ni Wingi wa Uzalishaji pamoja na kukidhi hitajio la huduma ya maji nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Majeshi Jenerali John Mkunda ametoa shukurani kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kumpa heshima ya kushiriki tukio hilo la kihistoria lenye lengo la Kukuza Uchumi nchini.

“Niwapongeze SUMAJKT kwa Ujumla kwa namna mnavyojitahidi kuboresha miundo mbinu ya makampuni, viwanda na miradi ili kuongeza Uzalishaji wenye tija na namna mnavyoshiriki majukumu mbalimbali ya kijamii hii ni ishara ya kuliletea Heshima Jeshi kwa Ujumla”

Aidha Jenerali Mkunda ameendelea kusema: “Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais Samia ina matarajio Makubwa kwa Jeshi hasa JKT na SUMAJKT kwa namna mnavyotekeleza miradi mikubwa ya kitaifa kwa weledi na kwa wakati”

Kadhalika Jenerali Mkunda amesema kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na JKT Kupitia SUMAJKT kutekeleza MRADI wa ofisi ya Rais Ikulu ya Chamwino na Mji wa kiserikali mtumba jijini Dodoma na sasa limepewa jukumu lingine la Ujenzi wa Nyumba 5000 za makazi ya wananchi wanaopisha eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia katika Kijiji cha msomera Handeni Jijini Tanga, ni dhahiri kuwa wameaminiwa kupewa miradi mikubwa ya nchi.

Akizungumzia kuhusu huduma ya Uzalishaji itakayoanza kufanyika sasa Jenerali Mkunda amewasihi SUMAJKT kupitia kiwanda hicho kufanya Uzalishaji wenye faida ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama katika kuzalisha maji.

Sambamba na uzinduzi wa mitambo hiyo, Jenerali Mkunda pia Amezindua magari mapya yatakayotumika katika usambazaji wa maji kwa wateja, ambapo magari hayo ambapo magari hayo yamenunuliwa na SUMAJKT.

Naye Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Hassan Mabena Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amemshukuru Jenerali Mkunda kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa mitambo ya kiwanda ambacho kina takribani miaka sita tangu kuanzishwa kwake.

“kiwanda kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na uhafifu wa Uzalishaji hali iliyopelekea shirika kuona umuhimu wa kufanya maboresho ili kuongeza Uzalishaji na mapato kwa shirika”

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema tukio hilo ni adhma ya kutimiza malengo ya shirika ya kuboresha, viwanda vingine, makampuni, na Miradi mbalimbali ili kukuza shirika kiuchumi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Maafisa Jenerali, wakuu wa matawi , Wakurugenzi wa SUMAJKT na JKT kwa ujumla, Wakuu wa MIRADI, wakuu wa shule, Vyuo, Baadhi ya wakuu wa vikosi, wajumbe wa Bodi ya SUMAJKT, pamoja na watendaji wa SUMAJKT, na Waandishi wa habari.

Similar Posts

  • SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

    SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…

  • Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane

    Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kuboresha Maonesho ya Wakulima Nanenane katika Banda la JKT. Dkt. Serera ametoa pongezi hizo leo tarehe 6 Agost 2025, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa Nzuguni Dodoma. Vilevile, Dkt. Serera amefurahishwa na Ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa na Huduma zinazotolewa na JKT pamoja na Shirika lake la SUMAJKT. Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa…

  • Waziri wa Ulinzi Zimbabwe atembelea SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Oppah Kashiri, amefanya ziara Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mlalakuwa Dar es salaam. Katika Ziara hiyo Mhe. Waziri Kashiri, akiwa na Waziri wa Ulinzi na JKT wa Tanzania Dkt. Stergomena Tax, alipatiwa taarifa ya shirika na kutembelea kiwanda cha Taa cha SUMAJKT Skyzone Co Ltd. Kilichopo Mlalakuwa na kiwamda cha Maji ya Kunywa cha SUMAJKT Bottling Co Ltd. Kilichopo Mgulani JKT.

  • Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT awaasa watendaji juu ya vihatarishi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema, kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa vihatarishi katika utendaji, Shirika limeamua kufanya mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watendaji ili kuwajengea uwezo katika kutambua, kutathimini na kudhibiti vihatarishi kwa lengo la kuleta tija katika utendaji. Brigedia Jenerali Ngata, amezungumza hayo Machi 4, 2026 katika ukumbi wa Umoja unaosimamiwa na SUMAJKT Catering Co.Ltd uliopo Mwenge Dar es Salaam.

  • Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT

    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi…

  • SUMAJKT, NYUMBU NA MZINGA KUENDELEZA USHIRIKIANO

    Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo. Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam. Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga….

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *