JENERALI MKUNDA AZINDUA MITAMBO YA MAJI SUMAJKT BOTTLING CO. LTD, AFURAHISHWA NA JITIHADA ZA SHIRIKA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 16 Oktoba 2023 amezindua mitambo ya kuzalisha Maji ya kunywa ya Uhuru Peak katika kiwanda cha SUMAJKT Bottling Co. Limited kilichopo Mgulani JKT Jijini Dar es salaam.

Mitambo hiyo yenye thamani ya Tsh Bilioni Moja na milioni 800 inaanza kutumika rasmi kuanzia sasa ili kuongeza ufanisi wa kiwanda ikiwa ni Wingi wa Uzalishaji pamoja na kukidhi hitajio la huduma ya maji nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Majeshi Jenerali John Mkunda ametoa shukurani kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kumpa heshima ya kushiriki tukio hilo la kihistoria lenye lengo la Kukuza Uchumi nchini.

“Niwapongeze SUMAJKT kwa Ujumla kwa namna mnavyojitahidi kuboresha miundo mbinu ya makampuni, viwanda na miradi ili kuongeza Uzalishaji wenye tija na namna mnavyoshiriki majukumu mbalimbali ya kijamii hii ni ishara ya kuliletea Heshima Jeshi kwa Ujumla”

Aidha Jenerali Mkunda ameendelea kusema: “Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais Samia ina matarajio Makubwa kwa Jeshi hasa JKT na SUMAJKT kwa namna mnavyotekeleza miradi mikubwa ya kitaifa kwa weledi na kwa wakati”

Kadhalika Jenerali Mkunda amesema kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na JKT Kupitia SUMAJKT kutekeleza MRADI wa ofisi ya Rais Ikulu ya Chamwino na Mji wa kiserikali mtumba jijini Dodoma na sasa limepewa jukumu lingine la Ujenzi wa Nyumba 5000 za makazi ya wananchi wanaopisha eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia katika Kijiji cha msomera Handeni Jijini Tanga, ni dhahiri kuwa wameaminiwa kupewa miradi mikubwa ya nchi.

Akizungumzia kuhusu huduma ya Uzalishaji itakayoanza kufanyika sasa Jenerali Mkunda amewasihi SUMAJKT kupitia kiwanda hicho kufanya Uzalishaji wenye faida ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama katika kuzalisha maji.

Sambamba na uzinduzi wa mitambo hiyo, Jenerali Mkunda pia Amezindua magari mapya yatakayotumika katika usambazaji wa maji kwa wateja, ambapo magari hayo ambapo magari hayo yamenunuliwa na SUMAJKT.

Naye Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Hassan Mabena Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amemshukuru Jenerali Mkunda kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa mitambo ya kiwanda ambacho kina takribani miaka sita tangu kuanzishwa kwake.

“kiwanda kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na uhafifu wa Uzalishaji hali iliyopelekea shirika kuona umuhimu wa kufanya maboresho ili kuongeza Uzalishaji na mapato kwa shirika”

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema tukio hilo ni adhma ya kutimiza malengo ya shirika ya kuboresha, viwanda vingine, makampuni, na Miradi mbalimbali ili kukuza shirika kiuchumi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Maafisa Jenerali, wakuu wa matawi , Wakurugenzi wa SUMAJKT na JKT kwa ujumla, Wakuu wa MIRADI, wakuu wa shule, Vyuo, Baadhi ya wakuu wa vikosi, wajumbe wa Bodi ya SUMAJKT, pamoja na watendaji wa SUMAJKT, na Waandishi wa habari.

Similar Posts

  • SUMAJKT yazindua gari kuongeza ufanisi shule ya Kawawa

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa. Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla. Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari…

  • GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana…

  • Brig. Jen. Ngata awapongeza watendaji SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wa shirika kwa kuzalisha na kutoa huduma bora kupitia Kampuni tanzu za SUMAJKT. Brigedia Jenerali Ngata, ameongea hayo katika kikao cha tathimini cha shirika kilichofanyika Januari, 16, 2026 katika Ukumbi wa mkutano Makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Kanda za Ujenzi, Kampuni, Miradi na Shule.

  • SUMAJKT, NYUMBU NA MZINGA KUENDELEZA USHIRIKIANO

    Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo. Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam. Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga….

  • BRIGEDIA SHIJA LUPPI ATEMBELEA SHOWROOM YA SUMAJKT FURNITURE COMPANY

    Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Shija Lupi, ametembelea Eneo la Mauzo (Show room) la Kampuni ya Samani (SUMAJKT Chang’ombe Furniture Co.Ltd) lililopo karibu na Barabara ya Mwai kibaki Mlalakuwa Jijini Dar es salaam, tarehe 01 Disemba 2025 ili kuona Mwenendo wa biashara unavyoendelea. Brigedia Jenerali Lupi amepokelewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo Meja Hemed Mchwanga ambapo amemueleza kuwa Kasi ya wateja kununua Samani zinazozalishwa na Kampuni ya SUMAJKT imeongezeka mara dufu katika kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka. Kampuni ya Samani ya SUMAJKT imeendelea kuzalisha bidhaa Bora na…

  • |

    Brigedia Ngata azindua magari ya Usafi SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua magari matano yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni moja ya Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) Kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizindua magari hayo Leo tarehe 19 Novemba 2024, Brigedia Jenerali Petro Ngata ameeleza kuwa Menejimenti ya SUMAJKT imejiwekea mikakati ya kuendelea kuongeza vitendeakazi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT, Kapteni Rosemary…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *