GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT).

Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro.

Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania.

Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana kibiashara ikiwemo Kilimo, Mifugo, Ujenzi, Usafirishaji, Maghala na uhifadhi wa bidhaa.

Ugeni huo ulipata fursa ya kuona baadhi ya Huduma na Bidhaa za Shirika hilo kupitia Maonesho Maalumu yaliyoandaliwa Kwa ajili yao katika Viwanja vya Makao Makuu ya Shirika hilo.

Aidha, Ugeni huo pia umetembelea Kiwanda cha Kutengeneza Taa za LED (SUMAJKT Skyzone Co. Ltd), ambacho kinatengeneza Taa za kutumia katika Viwanja vya ndege, mpira, Barabarani, mtaani, na kwenye majengo.

“Tunamshukuru sana Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata kwa mapokezi mazuri, yote aliyotueleza pindi alipokuja Comoro tumeyaona na tumefurahi sana, tumeona SUMAJKT wanafanya Mambo mengi hivyo tutakaa na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara ili kuona ni maeneo gani tuanze kufanya kazi pamoja” amesema Mhe.Mze Mohamed Ibrahim.

Vilevile, Gavana amemshukuru Mkurugenzi wa SUMAJKT kwa kuwapa majibu ya ufumbuzi wa changamoto walizomueleza pindi alipotembelea nchini Comoro.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, amemshukuru Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mhe. Mze Mohamed, kwa kutembelea SUMAJKT na kufafanua kuwa ziara hiyo imetokana na ziara yake aliyofanya nchini Comoro hivi karibuni.

Brigedia Jenerali Ngata amebainisha kuwa ugeni huo umeridhishwa na shughuli zinazofanywa na SUMAJKT pia wameonesha nia ya dhati ya kushirikiana katika Biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT ameuhakikishia Ugeni huo kuwa Shirika lipo tayari kushirikiana kibiashara katika maeneo ambayo watayaona yanafaa Kwa maslahi ya nchi zote mbili Tanzania na Comoro.


Similar Posts

  • SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi

    SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi. Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) imezidi kujiimarisha kwa kununua mashine za kisasa za kufagia barabara ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Taasisi na Kampuni mbalimbali nchini. Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, leo tarehe 30 Aprili 2025 baada ya kuzindua Mashine za kisasa za kufagia barabara amewahimiza watendaji wa kampuni hiyo kutunza mashine hizo ili ziweze kuleta tija kwa shirika. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua uwepo wa Mashine hizo kutaiongezea kampuni hiyo uwezo zaidi…

  • Brigedia Jenerali Petro Ngata apokelewa kwa Furaha SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa Brigedia Jenerali Petro Ngata, amepokelewa kwa furaha na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano, Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Brigedia Jenerali Ngata akipokelewa kwa mara ya kwanza tangu apandishwe cheo hicho kutoka cheo cha Kanali, alianza kukaribishwa kwa gwaride la heshima na baadae kupokelewa na kamati ya Utendaji ya SUMAJKT. Akizungumza katika ukumbi wa mikutano Brigedia Jenerali Ngata ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu Meja Jenerali Rajab Mabele…

  • |

    BRIGEDIA JENERALI NGATA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYABIASHARA NCHINI COMORO

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi ka Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amefanya mazungumzo na Jumuiya ya wafanyabiashara kisiwani Comoro katika ukumbi wa Chambre de Commerce Ngazidja uliopo kisiwani humo. Kikao hicho kimefanyika tarehe 5 Septemba 2024, na wafanyabiashara wanaochukua bidhaa Tanzania na kuzipeleka nchini Comoro, Brigedia Jenerali Ngata alipata fursa ya kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT hususani katika Sekta ya Ujenzi, Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata ameeleza nia thabiti ya SUMAJKT kuhitaji kufanya kazi na wafanyabiashara hao katika nyanja ya Ujenzi na Kilimo. Kwa upande wa wafanyabiashara kisiwani Comoro wamesema…

  • DC IKUNGI AVUTIWA NA MAONESHO YA JKT NANE NANE

    DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe.Thomas Cornel amevutiwa na Bidhaa na Huduma za Jeshi la Kujenga Taifa katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma. Akizungumza baada ya kutembelea Banda la JKT leo tarehe 6 Agost 2025, Mhe. Cornel amepongeza JKT kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayosaidia upatikanaji wa chakula cha asili kinachokidhi viwango vya soko la kimataifa. DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Vilevile, Mhe. Cornel amepongeza JKT na Shirika lake SUMAJKT kwa Ubunifu wa bidhaa mbalimbali na Utekelezaji mzuri wa…

  • Brig. Jen. Ngata awapongeza watendaji SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wa shirika kwa kuzalisha na kutoa huduma bora kupitia Kampuni tanzu za SUMAJKT. Brigedia Jenerali Ngata, ameongea hayo katika kikao cha tathimini cha shirika kilichofanyika Januari, 16, 2026 katika Ukumbi wa mkutano Makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Kanda za Ujenzi, Kampuni, Miradi na Shule.

  • SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

    SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *