Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta

Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema shirika lina dhamira ya kuendelea kujitanua na kuimarisha miundombinu ya kimkakati ya biashara ikiwemo sekta ya nishati.

Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema hayo katika uzinduzi wa gari la kusafirishia mafuta la Kampuni ya SUMAJKT Logistiki leo tarehe 26 Mei 2025, Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam. Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta.

Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua gari hilo litaongeza ufanisi katika usambazaji wa nishati ya mafuta na kupunguza gharama za usafirishaji hivyo kuongeza mapato ya Shirika.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMAJKT Logistiki Meja Mhidini Nchimbi, amesema gari hilo litatumika kusafirishia wa mafuta na kusambaza kwenye vituo vya SUMAJKT Energies pamoja na vituo vya watu binafsi.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube

Similar Posts

  • WAZIRI WA ULINZI NA JKT AZINDUA BODI MPYA YA SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi ya shirika hilo iliyomaliza muda wake kwa kuweka mbele Ubunifu, Mikakati pamoja na kuibua Miradi mipya ya kiuwekezaji. Mhe. Waziri Rhimo Nyansaho, amezungumza hayo leo tarehe 14 Januari 2026 baada ya kuzindua Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino jijini Dodoma. Aidha, Mhe. waziri Nyansaho amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kwao na kutoa rai kwao kuendelea kusaidia SUMAJKT kusonga mbele na kufikia malengo…

  • SUMAJKT yazindua gari kuongeza ufanisi shule ya Kawawa

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa. Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla. Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari…

  • SUMAJKT yatembelewa na Ugeni kutoka Comoros

    Ugeni kutoka Kisiwa cha Comoro, tarehe 06 Septemba 23 umetembelea Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo Mlalakua jijini Dar es salaam. Ujumbe huo wa watu watano ukiongozwa na Mhe. Gavana Sitti Farouata Mhoudine umefika Makao Makuu ya SUMAJKT kwa ziara ya kikazi na umepokelewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Mhe. Gavana Sitti Farouata katika ziara hiyo amepata fursa ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT kupitia Taarifa fupi iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa SUMAJKT. Luteni Kanali George Wang’ombe.Taarifa hiyo…

  • MAAFISA JKT WAMEASWA KUTEKELEZA KWA WELEDI JUKUMU LA MALEZI YA VIJANA

    Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana. Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amewaasa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutekeleza kwa weledi jukumu la Malezi ya Vijana. Kanali Mrai ametoa rai hiyo tarehe 21 Machi 2025 wakati akihitimisha Semina Elekezi ya Maafisa wa JWTZ waliopewa Uhamisho kwenda JKT, iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiendesha Semina Elekezi kwa watendaji wake ili kuwajengea uwezo wa…

  • Waziri wa Ulinzi Angola, aridhishwa na shughuli za SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameridhishwa na shughuli zinazofanywa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT). Akizungumza baada ya kufanya ziara SUMAJKT leo tarehe 11 Januari 2025, Mhe. Dos Santos, amebainisha kuwa amevutiwa na uzalishaji unaofanywa na Shirika hilo, hivyo wataenda kufanyiakazi nchini kwao. “Wizara yetu ya Ulinzi nchini Angola kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania tutakuja kusaini hati ya awali ya makubaliano ambayo itaonesha maeneo ya kushirikiana” alisema Mhe. Dos Santos. Aidha, Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania kupitia JWTZ kwa kuwezesha…

  • Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja atembelea SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim atembelea SUMAJKT akiangalia Bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata alimpokea Gavana wa Ngazidja Mze Mohamed Ibrahim baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), tarehe 05 Octoba 2024. Ambapo Ugeni huo Ulikuja Tanzania kwa ajili ya Mahusiano ya kibiashara na SUMAJKT. Akiambatana na ujumbe kutoka Comoro, Gavana alipata wasaa wa kutembelea na kujionea bidhaa mbalimbali katika Banda la Maonesho ya Bidhaa na Huduma alipotembelea Makao Makuu ya shirika…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *