DKT. STERGOMENA TAX AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI ENEO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA KIKOMBO DODOMA
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 31 Januari 2025, amewaongoza Maafisa, Askari, Vijana na Watumishi wa Umma katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo pamoja na eneo la viwanja vya makazi ya watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Chinangali 2 nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema zoezi hilo ni muendelezo wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Samia…


