Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa atuma salamu za Sikukuu kwa kuwatakia Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wa umma Heri ya Pasaka.
Similar Posts
SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba
SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…
SUMAJKT Kutafuta Fursa za Biashara visiwani Comoro
Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi. Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata. Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha…
RUVU JKT WAACHANA NA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA
Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax ameupongeza uongozi wa kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mkoani Pwani kwa kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati ya gesi kwa asilimia 100. Ruvu JKT waachana na matumizi ya kuni na mkaa. Mhe.Dkt. Tax ametoa pongezi hizo tarehe 3 Aprili 2025 wakati alipofanya ziara kikosini hapo na kujionea namna kikosi hicho chini ya Uongozi wa kamanda kikosi Kanali Peter Mnyani unavyotekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa Taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100. Amepongeza ubunifu wa…
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT. Mkuu wa Tawi la Mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Longinus Nyingo tarehe 16 Aprili 2025 amekagua Maandalizi ya Mwisho kuelekea kuhitimishwa kwa zoezi la Ufungaji wa Mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano katika Kikosi cha Ruvu JKT Mlandizi mkoani Pwani. Kanali Nyingo amesema kuwa, zoezi la ufungaji wa Mafunzo katika Vikosi vyote vya JKT lilianza tarehe 8 Aprili 2025 ambapo Mkuu wa JKT alikuwa akiwakilishwa na Wakuu wa Matawi…
Washiriki wa Kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Mataifa 16 Duniani wamefanya ziara ya Kimafunzo Makao Makuu ya JKT
Washiriki wa Kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Mataifa 16 Duniani wamefanya ziara ya Kimafunzo Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma mnamo Machi 10, 2025. Wakiwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamepata wasilisho la Namna JKT na Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) linavyotekeleza majukumu yake ya Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali na Ulinzi. https://www.instagram.com/p/DHBmQZOIPxl/?igsh=cXZmNjdhZGp1ZDFw Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube


