Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa

Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amewataka Wakurugenzi Waendeshaji, Wakuu wa Shule na Miradi kutumia vizuri fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija kwa Shirika.

Brigedia Jenerali Ngata ameyasema hayo tarehe 15 Agosti 2025 katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Brigedia Jenerali Ngata amehimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Shirika.

Aidha, amewasisitiza kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma katika ubora ili kuendelea kuilinda imani ya wananchi waliyonayo kwa SUMAJKT.

Vilevile amewakumbusha kuendelea kutekeleza Majukumu yao kwa Weledi na Uaminifu.

Brigedia Jenerali Ngata amehitimisha Kikao hicho kwa kuwapongeza Wakurugenzi Waendeshaji wa Kampuni Tanzu za SUMAJKT, na Wakuu wa Shule wanaofanya vizuri na kuwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi ili Shirika lizidi kusonga mbele.

Kamati ya Utendaji SUMAJKT hufanya Kikao kila mwezi kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za Uzalishaji Mali zinazofanywa na Shirika hilo.

Similar Posts

  • DED SUMAJKT atembelea Mafinga.

    DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa. Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi. Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea…

  • Waziri wa Ulinzi Angola, aridhishwa na shughuli za SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameridhishwa na shughuli zinazofanywa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT). Akizungumza baada ya kufanya ziara SUMAJKT leo tarehe 11 Januari 2025, Mhe. Dos Santos, amebainisha kuwa amevutiwa na uzalishaji unaofanywa na Shirika hilo, hivyo wataenda kufanyiakazi nchini kwao. “Wizara yetu ya Ulinzi nchini Angola kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania tutakuja kusaini hati ya awali ya makubaliano ambayo itaonesha maeneo ya kushirikiana” alisema Mhe. Dos Santos. Aidha, Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania kupitia JWTZ kwa kuwezesha…

  • JENERALI MKUNDA AZINDUA MITAMBO YA MAJI SUMAJKT BOTTLING CO. LTD, AFURAHISHWA NA JITIHADA ZA SHIRIKA

    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 16 Oktoba 2023 amezindua mitambo ya kuzalisha Maji ya kunywa ya Uhuru Peak katika kiwanda cha SUMAJKT Bottling Co. Limited kilichopo Mgulani JKT Jijini Dar es salaam. Mitambo hiyo yenye thamani ya Tsh Bilioni Moja na milioni 800 inaanza kutumika rasmi kuanzia sasa ili kuongeza ufanisi wa kiwanda ikiwa ni Wingi wa Uzalishaji pamoja na kukidhi hitajio la huduma ya maji nchini. Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Majeshi Jenerali John Mkunda ametoa shukurani kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika…

  • Meja Jen. Mabele aikaribisha SUA Makao Makuu ya JKT Dodoma.

    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameukaribisha Makao Makuu ya JKT Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ili kufanya mazungumzo ya namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo ndani Jeshi la Kujenga Taifa. Meja Jenerali Mabele ametoa ukaribisho huo leo tarehe 31 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, baada ya kufanyika kikao cha Utekelezaji wa Makubaliano kati ya JKT na SUA juu ya Mpango wa Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo hicho. Nae Dkt. Nyambelila Amouri kutoka RASI NDAKI ya Kilimo SUA mkoani Morogoro amesema, kupitia kikao hicho na ushirikiano uliopo…

  • Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT awaasa watendaji juu ya vihatarishi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema, kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa vihatarishi katika utendaji, Shirika limeamua kufanya mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watendaji ili kuwajengea uwezo katika kutambua, kutathimini na kudhibiti vihatarishi kwa lengo la kuleta tija katika utendaji. Brigedia Jenerali Ngata, amezungumza hayo Machi 4, 2026 katika ukumbi wa Umoja unaosimamiwa na SUMAJKT Catering Co.Ltd uliopo Mwenge Dar es Salaam.

  • Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT

    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *