|

KAMISHNA WA JKT KUTOKA NCHINI NAMIBIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA SUMAJKT

Kamishna wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Namibia Dkt. Felix Masukubili amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Leo tarehe 18 Novemba 2024 Mlalakuwa Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Masukubili amepokelewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji Kanali Festus Mang’wela.

Akiwa katika ziara hiyo amejionea shughuli za uzalishaji Mali zinazofanywa na SUMAJKT ikiwemo kiwanda cha kutengeneza Taa cha SUMAJKT SKYZONE CO.LTD ambacho kinazalisha taa zinazotumia nishati ya jua na umeme, kilichopo Mlalakuwa Makao Makuu ya SUMAJKT.

Dkt. Masukubili alipata fursa ya kutembelea pia kiwanda cha kuzalisha Maji ya kunywa cha SUMAJKT Bottling Co. Ltd na kiwanda cha Ushonaji cha SUMAJKT Garment Co. Ltd vilivyopo Mgulani JKT.

Similar Posts

  • | | |

    WANANCHI WA COMORO WAFURAHISHWA NA BIDHAA KUTOKA SUMAJKT

    Tarehe 12 hadi 19 mwezi Disemba 2022 kulifanyika Maonyesho ya Kibiashara eneo la ETG Moroni ambapo maonyesho hayo yaliratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro. Katika maonyesho hayo SUMAJKT ilialikwa kwa ujumbe rasmi wa balozi na uwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed. Maonyesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya serikali na wananchi wa nchi hizo mbili (Tanzania na Comoro) ambapo wananchi Comoro wafurahishwa na bidhaa kutoka SUMAJKT. Wananchi wa Moroni walipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozakishwa na SUMAJKT na wengi walionyesha kuridhishwa na viwango vya bidhaa hizo. Katika picha unaweza kushuhudia…

  • Waziri Kabudi aridhishwa na Ujenzi wa viwanja kwa ajili ya CHAN.

    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Palamagamba Kabudi (Mb) ameridhishwa na kazi inayofanywa na Kampuni ya SUMAJKT Construction Company Ltd, katika ujenzi wa viwanja vya mazoezi kwa ajili michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) yatakayofanyika mwezi Februari mwaka 2025. Katika Ukaguzi huo Profesa Kabudi, amefafanua kwamba viwanja hivyo vitakamilika ifikapo tarehe 21 Januari 2025 kwa ajili ya kuanza kutumika kwa mazoezi ya michuano ya CHAN. Nae Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, kwa niaba JWTZ ameeleza kwamba JKT limekabidhiwa kazi hivyo litaitekeleza kazi hiyo kwa muda uliopangwa….

  • |

    BRIGEDIA JENERALI NGATA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYABIASHARA NCHINI COMORO

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi ka Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amefanya mazungumzo na Jumuiya ya wafanyabiashara kisiwani Comoro katika ukumbi wa Chambre de Commerce Ngazidja uliopo kisiwani humo. Kikao hicho kimefanyika tarehe 5 Septemba 2024, na wafanyabiashara wanaochukua bidhaa Tanzania na kuzipeleka nchini Comoro, Brigedia Jenerali Ngata alipata fursa ya kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT hususani katika Sekta ya Ujenzi, Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata ameeleza nia thabiti ya SUMAJKT kuhitaji kufanya kazi na wafanyabiashara hao katika nyanja ya Ujenzi na Kilimo. Kwa upande wa wafanyabiashara kisiwani Comoro wamesema…

  • Nyumba 5000 zakamilika Msomera

    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujemga Taifa SUMAJKT, Kupitia Kampuni ya Ujenzi ya @sumajktccl limekamilisha awamu ya Kwanza ya Mradi wa Nyumba 2500 katika Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Mkoani Tanga. Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji iliyotumika kukamilisha nyumba hizo. Taarifa zaidi tizama video hii hapa chini..

  • |

    Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi

    Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Daniel Sillo ayashauri mashirika ya Kijeshi ndani ya Nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Sayansi na Teknolojia katika uzalizalishaji wa bidhaa zao. Mhe. Sillo amesema hayo leo tarehe 25 Februari 2025 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mashirika yanayo milikiwa na  Majeshi ya  nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Geraffe iliyopo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi, Amefafanua kuwa Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Viwanda vilivyopo ndani ya Majeshi yaliyopo katika Jumuiya ya…

  • |

    Brigedia Ngata azindua magari ya Usafi SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua magari matano yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni moja ya Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) Kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizindua magari hayo Leo tarehe 19 Novemba 2024, Brigedia Jenerali Petro Ngata ameeleza kuwa Menejimenti ya SUMAJKT imejiwekea mikakati ya kuendelea kuongeza vitendeakazi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT, Kapteni Rosemary…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *