Habari na Matukio

  • Brig. Ngata awataka Wakurugenzi kuongeza Ubunifu

    Brig. Ngata awataka Wakurugenzi kuongeza Ubunifu. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewataka Wakurugenzi waendeshaji wa Viwanda vya Uzalishaji Maji, Ushonaji na Shule ya Sekondari Jitegemee vilivyopo Mgulani JKT kuongeza ubunifu katika Uendeshaji wa Miradi ya kiuchumi na yenye tija kwa Taifa. Brigedia Jenerali Ngata, amesema hayo Oktoba 03, 2025 alipotembelea viwanda pamoja na shule ya Jitegemee kwa lengo la kuona maendeleo ya viwanda hivyo vilivyopo mgulani JKT jijini Dar es Salaam. Aidha, Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema Makao Makuu ya Shirika inaendelea kuboresha Viwanda, Kampuni, Miradi na Shule…

  • Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT

    Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu Nchini Namibia Meja jenerali Aktofel Nambahu Amevutiwa na Shughuli za Uzalishaji mali zinazofanya na Jeshi la Kujenga Taifa Kupitia Shirika lake SUMAJKT. Meja Jenerali Nambahu amepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele leo tarehe 20 Agosti 2025 Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Jijini Dar es salaam. Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT. Ziara yangu JKT ni mualiko wa Mkuu…

  • Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa

    Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amewataka Wakurugenzi Waendeshaji, Wakuu wa Shule na Miradi kutumia vizuri fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija kwa Shirika. Brigedia Jenerali Ngata ameyasema hayo tarehe 15 Agosti 2025 katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho Brigedia Jenerali Ngata amehimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Shirika. Aidha, amewasisitiza kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma katika…

  • Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane

    Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kuboresha Maonesho ya Wakulima Nanenane katika Banda la JKT. Dkt. Serera ametoa pongezi hizo leo tarehe 6 Agost 2025, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa Nzuguni Dodoma. Vilevile, Dkt. Serera amefurahishwa na Ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa na Huduma zinazotolewa na JKT pamoja na Shirika lake la SUMAJKT. Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa…

  • DC IKUNGI AVUTIWA NA MAONESHO YA JKT NANE NANE

    DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe.Thomas Cornel amevutiwa na Bidhaa na Huduma za Jeshi la Kujenga Taifa katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma. Akizungumza baada ya kutembelea Banda la JKT leo tarehe 6 Agost 2025, Mhe. Cornel amepongeza JKT kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayosaidia upatikanaji wa chakula cha asili kinachokidhi viwango vya soko la kimataifa. DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Vilevile, Mhe. Cornel amepongeza JKT na Shirika lake SUMAJKT kwa Ubunifu wa bidhaa mbalimbali na Utekelezaji mzuri wa…