Habari na Matukio

  • DC IKUNGI AVUTIWA NA MAONESHO YA JKT NANE NANE

    DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe.Thomas Cornel amevutiwa na Bidhaa na Huduma za Jeshi la Kujenga Taifa katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma. Akizungumza baada ya kutembelea Banda la JKT leo tarehe 6 Agost 2025, Mhe. Cornel amepongeza JKT kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayosaidia upatikanaji wa chakula cha asili kinachokidhi viwango vya soko la kimataifa. DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Vilevile, Mhe. Cornel amepongeza JKT na Shirika lake SUMAJKT kwa Ubunifu wa bidhaa mbalimbali na Utekelezaji mzuri wa…

  • Mwenyekiti kamati ya NaneNane akaribisha wananchi Dodoma

    Mwenyekiti kamati ya NaneNane akaribisha wananchi Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wakulima Nanenane Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Shija Lupi amewakaribisha wananchi wote hapa nchini kutembelea Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma na Kikanda katika Kanda zote ambazo Jeshi hilo linashiriki.

  • SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

    SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…

  • Wanafunzi kutoka Nigeria wafurahishwa na shughuli za SUMAJKT

    Wanafunzi kutoka Nigeria wafurahishwa na shughuli za SUMAJKT. Ugeni wa Wakufunzi na wanafunzi chuo Cha Taifa Cha Mafunzo ya Usalama nchini Nigeria wafurahishwa na Shughuli za Jeshi la Kunega pamoja na Shirika lake SUMAJKT. Ugeni huo wa Wakufunzi na wanafunzi idadi 25 ukiongozwa na Mkuu wa Msafara huo Makamu Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo Bwana Hyginus Ngele Umepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa jijini Dar es salaam tarehe…

  • Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta

    Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema shirika lina dhamira ya kuendelea kujitanua na kuimarisha miundombinu ya kimkakati ya biashara ikiwemo sekta ya nishati. Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema hayo katika uzinduzi wa gari la kusafirishia mafuta la Kampuni ya SUMAJKT Logistiki leo tarehe 26 Mei 2025, Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam. Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua gari hilo litaongeza ufanisi katika usambazaji wa nishati ya…